Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Katika kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, wanawake wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Tanga wameadhimisha siku hiyo kwa kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha FURAHA, kilichopo Raskazone, jijini Tanga, na kutoa msaada wa mahitaji muhimu kama unga, mchele, mafuta, sabuni za kufulia na za kuogea. Baada ya kukabidhi vitu hivyo, watoto hao walionyesha furaha na shukurani zao kupitia nyimbo na michezo mbalimbali.
Maadhimisho haya hufanyika kila tarehe 08 Machi. Mwaka huu, yalikuwa na kaulimbiu isemayo: “Haki ya Mwanamke na Wasichana, Msingi wa Maendeleo Jumuishi Kufikia Dira 2050.”
Akizungumza kwenye tukio hilo kwa niaba ya wanawake wa NIMR Tanga, Dr. Veneranda Bwana alisema ni desturi ya wanawake wa NIMR kushiriki katika masuala ya jamii, na akasisitiza kwamba kila siku ni fursa ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wengine. “Siku ya Wanawake Duniani ni fursa ya kusherehekea wanawake, lakini pia ni wakati wa kuonyesha mshikamano na wale walioko kwenye hali ngumu,” alisisitiza Dr. Bwana.
Msimamizi wa kituo hicho aliwashukuru wanawake wa NIMR Tanga kwa msaada huo na akakaribisha wadau mbalimbali kuendeleza jitihada za kutoa misaada, akibainisha kwamba watoto hao wanahitaji msaada ili kuendeleza maisha yao.

Section Title

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu

Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limewataka watafiti kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika vituo vya Taasisi kuongeza machapisho na ubunifu wa utafiti, ili...

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya

Serikali imetoa wito kwa watafiti na wadau wa tiba asili kuongeza kasi ya tafiti, uthibitishaji wa kisayansi na uwekezaji katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, ili zenye ushahidi wa usalama, ubora...

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

NIMR to Lead Ethical Oversight in a Multicountry Trial Exploring New Approaches to Prevent Childhood Diarrhoeal Diseases.

The National Institute for Medical Research (NIMR) is leading ethical oversight in a new multicountry clinical trial investigating whether probiotics can enhance the protection provided by rotavirus...

NIMR TABORA RESEARCH CENTRE A CENTURY OF SCIENCE: A NEW ERA OF PUBLIC HEALTH IMPACT

From a Sleeping Sickness Unit to a Modern Public Health Research Hub For more than a century, NIMR Tabora has connected scientific discovery with practical public health action. Established in Tabora...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

NIMR and HJF Strengthen Health Research Collaboration

The National Institute for Medical Research (NIMR) and the U.S.-based Henry M. Jackson Foundation (HJF) have discussed strategies to strengthen the existing collaboration in health research including...

NIMR and Museen Stade Strengthen Strategic Partnership to Advance Research, Heritage and Tourism at Amani Hill

The National Institute for Medical Research (NIMR) and Museen Stade of Germany have formalized their partnership through the signing of a collaboration agreement under the WAYS – Towards Fair and...

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Dira 2050