Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Uncategorized

CONGRATULATIONS

The National Institute for Medical Research (NIMR) extends its heartfelt congratulations to Dr. Nyanda Elias Ntinginya on his selection as a 2026 Kofi Annan Fellow in Global Health Leadership. The Kofi Annan Fellowship in Global Health Leadership, implemented by Africa CDC in partnership with the Kofi Annan Foundation, is a distinguished continental leadership programme that equips senior public health professionals from African Union Member States with advanced competencies in strategic leadership, health diplomacy, policy influence, and health systems transformation to strengthen public health systems across Africa. Dr. Ntinginya’s selection reflects his professional excellence, leadership, and continued commitment to advancing public health research and strengthening health systems across the continent. We wish you every success throughout the fellowship programme. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

CONGRATULATIONS Read More »

NIMR Launches DIMENSION Project to Advance Digital Innovation in Mental Health Care for People Living with HIV

NIMR Muhimbili Centre has launched DIMENSION (Digital Empowerment for Mental Health in Tanzania: Enhancing Healthcare Capacity through Innovative Digital Training Solutions for People Living with HIV), a new project aimed at bringing digital innovation to mental health care for people living with HIV in Tanzania. The project brings together NIMR Muhimbili Centre, the Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS), and the University of Copenhagen–Psychiatry Centre to strengthen mental health care capacity through innovative digital training solutions and equitable partnerships. Through capacity building, DIMENSION project seeks to address challenges in mental health care and advance the use of digital solutions to support mental health services. The project also aims to develop a replicable digital tool (a digital solution that can be used in other settings with similar needs and resource constraints) to improve mental health screening, education and service delivery in low-resource settings. The initiative contributes to ongoing efforts to connect research, digital innovation and health-system capacity building to strengthen mental health care for people living with HIV in Tanzania. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR Launches DIMENSION Project to Advance Digital Innovation in Mental Health Care for People Living with HIV Read More »

NIMR Receives Bioinformatics Equipment to Advance Health Research and Genomic Data Analysis

The National Institute for Medical Research (NIMR) has received bioinformatics equipment and systems from AMREF Health Africa Tanzania to advance health research and genomic data analysis, while strengthening the Institute’s capacity to generate evidence for disease surveillance, outbreak preparedness and public health decision making.The equipment was officially handed over on 14th September 2026, at the NIMR sub-Office in Dar es Salaam and includes genomic analysis software, information technology equipment and office furniture for the NIMR Bioinformatics Laboratory.Speaking at the handover ceremony, NIMR Director General, Prof. Said S. Aboud, said the contribution represents an investment in scientific capacity, innovation and NIMR ability to generate high-quality evidence to improve health in Tanzania and beyond.Prof. Aboud said the equipment will strengthen NIMR capacity to undertake advanced bioinformatics analyses and support the application of genomic technologies in health research, disease surveillance, outbreak preparedness and response, and public health decision-making. He added that it will also provide researchers, bioinformaticians, laboratory scientists and trainees with improved access to infrastructure needed for modern genomic research and analysis, contributing to the development of the next generation of Tanzanian scientists.The equipment was acquired through AMREF Health Africa Tanzania’s Global Health Security Agenda II (GHSA II) Project, funded by the U.S. Government through CDC Tanzania, to strengthen genomic data analysis infrastructure and national health security capacity.AMREF Health Africa Tanzania Country Director, Dr. Florence Temu, said the equipment will support genomic data analysis and research on infectious and non-communicable diseases, as well as to contribute to the early detection of emerging pathogens.She added that improved genomic data analysis will also support Precision Medicine through better understanding of genetic information to inform treatment approaches.The equipment handed over includes a Geneious Software License for genomic analysis, two Lenovo laptops, an HP ProLiant Server, an Uninterruptible Power Supply (UPS), two office desks and two office chairs, with a total value of TZS 108,051,419.Dr. Temu emphasized the importance of NIMR to ensure proper use and maintenance of the equipment to sustain the benefits of the contribution and strengthen long-term national capacity in genomic data analysis.The handover reflects the value of collaboration between NIMR, AMREF Health Africa Tanzania and the U.S. Government through CDC Tanzania in strengthening scientific infrastructure and expertise needed to detect, monitor and respond to health threats. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR Receives Bioinformatics Equipment to Advance Health Research and Genomic Data Analysis Read More »

NIMR YAONYESHA MATUMIZI YA UTAFITI KUBORESHA HUDUMA ZA VVU KWA MAMA NA MTOTO

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umeonesha kwamba upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua unaweza kusaidia kuwatambua mapema mama na watoto walio katika hatari kubwa ya maambukizi, huku ubunifu wa kidijitali ukichangia kuboresha upatikanaji wa majibu ya vipimo katika vituo vya huduma za afya.Ushahidi huo umetokana na miradi ya LIFE na LIFE2Scale inayofadhiliwa na EDCTP, iliyolenga kuboresha huduma kwa wajawazito wanaoishi na VVU na watoto walio katika hatari ya kuambukizwa. Matokeo hayo yaliwasilishwa tarehe 10 Septemba 2026 katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi 2026, uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kwa ajili ya kuwafikishia watunga sera na wadau wa afya ushahidi wa kuendeleza maboresho ya miongozo na huduma za afya. Akifungua mjadala huo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said S. Aboud, amesema tafiti hizo zimeonesha umuhimu wa upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua katika kuwatambua walio katika hatari kubwa ya maambukizi na kuhakikisha wanaohitaji huduma wanafikiwa mapema.Prof. Aboud amesema NIMR imefanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, TAMISEMI na wadau, huku ikitumia na kuimarisha mifumo ya kitaifa iliyopo badala ya kuanzisha mifumo sambamba. Naye Mtafiti Mkuu wa LIFE2Scale, Dkt. Issa Sabi, amesema utafiti wa LIFE uliofanyika Tanzania na Msumbiji kati ya mwaka 2019 na 2022 ulionesha kuwa upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua unaweza kutambua mama na watoto wengi zaidi walio katika hatari kubwa ya maambukizi kuliko kutegemea vigezo vya kitabibu pekee. Amesema LIFE2Scale ilijengwa juu ya ushahidi huo kwa kuingiza ubunifu huo katika huduma za kawaida na kuimarisha mifumo ya kitaifa ikiwemo Electronic Sample Referral System (ESRS) na Unified Dkt. Sabi amesema utekelezaji wa LIFE2Scale katika vituo vya afya vya Mbeya na Songwe umechangia kuboresha mifumo ya utoaji huduma, ikiwemo kuongeza uwezo wa upimaji kupitia ununuzi wa takribani mashine 15 za GeneXpert kwa ajili ya upimaji wa VVU kwa watoto wachanga na magonjwa mengine, ikiwemo kifua kikuu. Amesema NIMR imewasilisha matokeo hayo kwa watunga sera na wadau wa afya ili kuchochea matumizi mapana ya ushahidi huo na kuendeleza maboresho yaliyopatikana katika maeneo yaliyoshiriki utafiti. Killian Mlalama alieleza namna Unified Community System–Kituoni App (UCS-Kituoni), iliyounganishwa na ESRS, ilivyosaidia kupunguza utegemezi wa majibu ya vipimo kwa njia ya karatasi na kuchangia kuboresha muda wa upatikanaji wa majibu, hususan katika vituo vya huduma vinavyopokea huduma kutoka vituo vya upimaji. Kwa upande wa Wizara ya Afya, Dkt. Mukome Nyamhagatta, Mratibu wa Taarifa za Kimkakati katika Mpango wa Taifa wa Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT), amesema Serikali imeona manufaa makubwa ya utafiti huo katika kutoa ushahidi unaoweza kusaidia kuboresha miongozo ya utoaji wa huduma za afya, na kuishukuru NIMR kwa kuendelea kutekeleza miradi yenye ushahidi unaosaidia Tanzania kuboresha utoaji wa huduma.Amesema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upimaji wa VVU kwa watoto wachanga, lakini bado kuna umuhimu wa kuimarisha ufuatiliaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa wajawazito, upimaji wakati wa kujifungua, upimaji wa VVU katika vituo vya huduma na matumizi ya taarifa katika kuboresha huduma. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR YAONYESHA MATUMIZI YA UTAFITI KUBORESHA HUDUMA ZA VVU KWA MAMA NA MTOTO Read More »

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu

Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limewataka watafiti kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika vituo vya Taasisi kuongeza machapisho na ubunifu wa utafiti, ili kuzalisha ushahidi unaochangia kuboresha afya ya Watanzania na sera za afya.Wito huo umetolewa tarehe 1 Septemba 2026, wakati Baraza lilipotembelea vituo vya NIMR Mabibo na Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea kwa vitendo shughuli na utendaji wa vituo hivyo, kutathmini matumizi ya miundombinu na vifaa vya utafiti, pamoja na kusikiliza maoni na changamoto za watumishi.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la NIMR, Prof. Muhammad Bakari Kambi, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Baraza, Prof. James Mdoe, alisema NIMR ina rasilimali watu wenye uwezo na miundombinu ya utafiti inayotoa fursa kwa watafiti kuongeza uzalishaji wa maarifa na machapisho, huku akiwasisitiza kutumia fursa hizo kuongeza mchango wa NIMR kitaifa na kimataifa.Prof. Kambi pia alisisitiza umuhimu wa kuongeza ubunifu katika tafiti na uzalishaji wa bidhaa za tiba asili, sambamba na kuimarisha masoko ya bidhaa hizo ili kuongeza matumizi na kuchangia mapato ya Taasisi. Aidha, aliwataka watumishi kutunza na kutumia kwa ufanisi uwekezaji wa Serikali katika miundombinu na vifaa vya utafiti, ikiwemo maabara na kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za tiba asili chenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 2.4.Katika ziara hiyo, Baraza lilitembelea maeneo mbalimbali ya vituo hivyo na kuona shughuli za utafiti, miundombinu na vifaa vinavyotumika katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi. Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni maabara za kituo cha NIMR Mabibo, shughuli za utafiti wa Kifua Kikuu na UKIMWI katika katika kituo cha NIMR Muhimbili, maabara ya Kifua Kikuu iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili inayosimamiwa na NIMR kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) pamoja na Wizara ya Afya, na Maabara ya Vinasaba vya Malaria iliyopo katika Ofisi ndogo za NIMR Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, alisema NIMR Mabibo ina maabara tatu zenye mashine zaidi ya 80 zinazotumika katika tafiti na ufuatiliaji wa ubora wa dawa za tiba asili. Alisema kituo hicho pia kina mitambo takribani 15 ya uzalishaji wa dawa, ambapo mitambo tisa tayari inafanya kazi na sita ikiwa katika hatua za usimikaji.Prof. Aboud alisema NIMR Mabibo imegundua bidhaa sita za tiba asili ambazo zipo katika hatua za awali, huku utafiti na majaribio yakiendelea. Kwa upande wa NIMR Muhimbili, alisema kituo hicho kimeendelea kutoa mchango katika kuboresha sera na miongozo mbalimbali ya afya nchini na kimataifa, ikiwemo katika maeneo ya VVU, Kifua Kikuu na magonjwa yanayohusiana nayo.Aliongeza kuwa NIMR Muhimbili inaendelea kuongeza machapisho kupitia ushirikiano na hospitali mbalimbali, matumizi ya kanzidata za tafiti za afya na tafiti za kimfumo zinazolenga kuunganisha ushahidi kutoka tafiti mbalimbali.Baraza pia lilipata fursa ya kukutana na watumishi wa vituo hivyo na kusikiliza maoni yao kuhusu utendaji wa kazi, changamoto wanazokabiliana nazo na maeneo yanayohitaji maboresho. Prof. Kambi aliwahakikishia watumishi kuwa changamoto zilizowasilishwa zitafanyiwa kazi, huku akiwapongeza kwa kazi wanayoifanya na kueleza kuridhishwa na maendeleo ya vituo hivyo.Ziara hiyo iliwezesha Baraza kupata uelewa wa moja kwa moja kuhusu shughuli, mafanikio, fursa na changamoto za vituo hivyo, pamoja na kutathmini maeneo yanayohitaji msukumo zaidi katika kuimarisha utendaji wa NIMR. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu Read More »

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya

Serikali imetoa wito kwa watafiti na wadau wa tiba asili kuongeza kasi ya tafiti, uthibitishaji wa kisayansi na uwekezaji katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, ili zenye ushahidi wa usalama, ubora na ufanisi ziweze kujumuishwa katika mfumo rasmi wa afya nchini.Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, katika Kongamano la Tano la Kisayansi la Tiba Asili lililofanyika leo, tarehe 28 Agosti 2026, katika Ukumbi wa Eden Highlands Hotel, Jijini Mbeya, ambapo alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu – Dawa na Vifaa Tiba wa Wizara ya Afya, Mhe. Emanuel Tayari, aliyekuwa Mgeni Rasmi.Balozi Dkt. Ulisubisya amesema Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili na maarifa ya tiba asili ambayo yanaweza kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto mbalimbali za afya, iwapo yatafanyiwa tafiti za kutosha na kuthibitishwa kisayansi.Amesema Serikali inahitaji kuona ongezeko la tafiti za tiba asili, uwekezaji katika maendeleo ya dawa hizo pamoja na kuimarika kwa uzalishaji katika viwanda vya ndani.Aidha, ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya wanasayansi, wataalamu wa tiba asili, wataalamu wa afya, taasisi za udhibiti, vyuo vikuu, watunga sera na sekta nyingine, ili kujenga mfumo unaowezesha tiba asili zenye ushahidi kutumika kwa usalama ndani ya huduma rasmi za afya.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la NIMR, Prof. James E. Mdoe, amesema maendeleo ya tiba asili yanahitaji kujenga daraja kati ya sayansi ya kisasa na maarifa ya jadi yaliyorithishwa na jamii kwa vizazi.Prof. Mdoe amesema Kongamano hilo ni fursa kwa watafiti, wataalamu wa tiba asili, watunga sera, watoa huduma za afya na wadau wengine kujadili ushahidi uliopo, changamoto na fursa za kuendeleza tiba asili nchini.Akizungumza katika Kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, amesema Taasisi hiyo kupitia Kituo cha Utafiti wa Tiba Asili Mabibo imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya maabara kwa ajili ya kuimarisha msingi wa kisayansi wa dawa za tiba asili.Prof. Aboud amesema maabara hizo tayari zinatumika kufuatilia ubora wa dawa 45 zinazopatikana kupitia mpango wa huduma jumuishi, ambapo dawa hizo zimewafikia zaidi ya wagonjwa 2,000 katika hospitali 14 za rufaa za mikoa.Prof. Aboud pia amesema NIMR inakamilisha taratibu za kuhakikisha Kiwanda cha Dawa za Tiba Asili Mabibo kinafunguliwa rasmi katika mwaka wa fedha 2026/27.Kongamano hilo, lenye kaulimbiu “Kuongeza Kasi ya Ujumuishaji wa Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Katika Mifumo Rasmi ya Afya: Jukumu la Ushirikiano wa Sekta Mbalimbali,” limewakutanisha wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala, watafiti, watoa huduma za afya, watunga sera, taasisi za udhibiti, vyuo vikuu na washirika wa maendeleo. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya Read More »

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya ukarabati wa Kituo Kidogo cha Utafiti cha NIMR Tukuyu yanakamilishwa.Prof. Mdoe ametoa kauli hiyo Agosti 27, 2026, wakati wa ziara ya siku moja katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya na Kituo Kidogo cha Utafiti cha NIMR Tukuyu, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli za utafiti zinazoendelea katika vituo hivyo pamoja na hali ya miundombinu na mazingira ya kazi.Akiwa Tukuyu, Prof. Mdoe alielezwa na uongozi wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya kuwa ukarabati wa kituo kidogo hicho unaendelea kwa kutumia vyanzo vya ndani vya mapato vya Taasisi. Prof. Mdoe alisisitiza umuhimu wa kukamilisha maeneo yaliyosalia ya ukarabati.Ziara hiyo pia ilimpa Prof. Mdoe fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za utafiti zinazofanyika katika vituo hivyo, ikiwemo tafiti za Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI katika Kituo cha NIMR Mbeya, pamoja na tafiti za ugonjwa wa Usubi zinazofanyika katika Kituo Kidogo cha Utafiti cha NIMR Tukuyu.Katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya, Prof. Mdoe alitembelea maabara za utafiti na kujionea matumizi ya mitambo ya kisasa kwa ajili ya shughuli za utafiti, pamoja na miundombinu ya kuhifadhi sampuli na majengo yanayotumika katika shughuli za kituo.Akizungumza na watumishi wa NIMR Mbeya na Tukuyu, Prof. Mdoe aliwatia moyo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii na weledi. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya kazi ili kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.Prof. Mdoe pia amewataka wananchi kushiriki katika tafiti zinazofanywa na NIMR, akieleza kuwa ushiriki wao ni muhimu katika kuwezesha tafiti kuzalisha ushahidi wa kisayansi unaoweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za afya zinazowakabili wananchi.Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya, Dkt. Bariki Mtafya, amemshukuru Prof. Mdoe kwa kutembelea vituo hivyo na kupata fursa ya kujionea shughuli za utafiti pamoja na changamoto zinazowakabili watafiti.Dkt. Mtafya amesema uongozi wa kituo utaendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kushughulikia changamoto mbalimbali na kuhakikisha shughuli za utafiti zinaendelea kwa ufanisi. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu Read More »

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za pamoja, kuimarisha uwezo wa watafiti na kutumia miundombinu iliyopo kupanua wigo wa tafiti nchini.Majadiliano hayo yalifanyika tarehe 13 Agosti 2026 katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya, wakati Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa HJF, Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Marekani, Dkt. Joseph Caravalho, pamoja na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, alisema kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani kunatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, hasa wakati ambapo mazingira ya ufadhili wa tafiti za afya duniani yanaendelea kubadilika.Prof. Aboud alisema NIMR imewekeza katika miundombinu ya utafiti katika Kituo cha Mbeya na vituo vyake vingine, ikiwemo maabara na vifaa vinavyowezesha tafiti mbalimbali za afya.Katika majadiliano hayo, pande hizo pia zilizungumzia mabadiliko katika ufadhili wa utafiti kutoka Marekani. Prof. Aboud alitoa shukrani kwa Serikali ya Marekani kwa mchango wake kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), ambao umeunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na changamoto nyingine za afya ya umma.NIMR na HJF pia zilijadili maeneo ya ushirikiano wa baadaye, yakiwemo kuendeleza tafiti za pamoja, kujenga uwezo wa watafiti na kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano wa kisayansi.Baada ya majadiliano, ujumbe wa HJF ulitembelea Maabara ya Usalama na Kinga ya Mwili (Safety and Immunology) ya Kituo cha NIMR Mbeya, ambapo ulijionea shughuli za utafiti zinazotekelezwa katika kituo hicho. Ujumbe huo pia ulielezwa kuhusu uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo HJF, katika kuimarisha miundombinu ya kituo.Ziara hiyo ilihitimishwa kwa pande zote mbili kueleza utayari wa kuendeleza ushirikiano uliopo na kutumia miundombinu na uwezo wa watafiti kupanua tafiti za afya nchini. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya Read More »

NIMR to Lead Ethical Oversight in a Multicountry Trial Exploring New Approaches to Prevent Childhood Diarrhoeal Diseases.

The National Institute for Medical Research (NIMR) is leading ethical oversight in a new multicountry clinical trial investigating whether probiotics can enhance the protection provided by rotavirus vaccination and reduce diarrhoeal disease among children. This approach could also help reduce antibiotic exposure and contribute to efforts to address antimicrobial resistance (AMR).The PRoRota Clinical Trial was launched in Dar es Salaam on 18th August 2026 by Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), in collaboration with NIMR and partners from Tanzania, Malawi, Côte d’Ivoire and Norway. The two-day kick-off meeting, held at White Sands Hotel, brought together researchers and partners from microbiology, infectious diseases, epidemiology, health economics, social sciences and public health.Speaking at the meeting, the Guest of Honour, Prof. Tumaini Nagu, Deputy Permanent Secretary in the Prime Minister’s Office responsible for Health, said childhood diarrhoeal diseases remain an important and preventable cause of illness and death among children. She highlighted the importance of research such as PRoRota in generating evidence on whether probiotics can strengthen the effectiveness of rotavirus vaccination, reduce diarrhoeal disease and potentially reduce antibiotic exposure and AMR. NIMR plays a key role in the consortium, including leading the Ethics Work Package to support ethical conduct and protection of infants that will participate in the trial across the three African countries. NIMR will also coordinate the project’s independent ethics oversight and Data Safety Monitoring Board. In addition, NIMR will co-lead the formative, acceptability and feasibility research, which will generate evidence on caregivers’, healthcare providers’ and other stakeholders’ perspectives and experiences to inform trial implementation and the potential future integration of probiotics into routine childhood immunization programmes.During opening remarks, the Director General Prof. Said Aboud reaffirmed NIMR commitment to ensuring that the trial is conducted in accordance with high ethical and scientific standards. He said the Institute will work closely with consortium partners to generate evidence that can contribute to improved prevention of childhood diarrhoeal diseases and inform future health decisions. The research will help establish not only whether the intervention works, but also how it may be received by caregivers and healthcare providers and if it can be implemented within participating healthcare systems.Childhood diarrhoeal diseases remain an important public health concern, while antibiotic use in managing infections adds to the broader challenge of AMR. By examining whether probiotics can strengthen the protection provided by rotavirus vaccination and potentially reduce antibiotic exposure, PRoRota seeks to generate evidence that could inform future approaches to childhood disease prevention and vaccination across the participating countries. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR to Lead Ethical Oversight in a Multicountry Trial Exploring New Approaches to Prevent Childhood Diarrhoeal Diseases. Read More »

Dira 2050