NIMR kupitia PEN-Plus Yafikisha Huduma za Magonjwa Yasiyoambukiza Karibu na Wananchi

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa utafiti wa PENPLUS imeendelea kuboresha utoaji wa huduma za magonjwa yasiyoambukiza nchini kwa kuwezesha Hospitali za Kondoa Mji na ya Kilutheri Karatu kutoa huduma za kibingwa ambazo awali zilipatikana katika hospitali za mikoa na rufaa pekee.Mafanikio hayo yamebainishwa wakati wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kimkakati wa Kikanda la PEN-Plus la Kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza Barani Afrika (3rd ICPPA 2026) linaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam, tarehe 23 hadi 25 Juni 2026.Akifungua Kongamano hilo, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema mkakati wa PEN-Plus umeendelea kuwa suluhisho muhimu barani Afrika katika kuimarisha huduma za magonjwa yasiyoambukiza kwa kuyasogeza karibu na wananchi, hususan katika hospitali za wilaya na vituo vya afya vilivyochaguliwa.Amesema kupitia ushirikiano kati ya Serikali, Washirika wa Maendeleo na Mpango wa Samia Suluhu Hassan Outreach, huduma za PEN-Plus zinaendelea kupanuliwa nchini kote, hasa katika maeneo ya vijijini na yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya.Akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya alipotembelea banda la NIMR, Mtafiti Kiongozi wa Mradi wa PEN-Plus nchini Tanzania, Dkt. Mary Mayige, alisema mradi huo wa utafiti umewezesha hospitali za Kondoa Mji na ya Kilutheri Karatu kutoa huduma za kibingwa za magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa afya, kuboresha miundombinu ya vituo vya kutolea huduma, pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa.Katika Kongamano hilo, NIMR inaendelea kutoa huduma za uchunguzi na ushauri wa afya kwa washiriki ikiwemo upimaji wa shinikizo la juu la damu, kisukari pamoja na vipimo vya urefu na uzito kwa lengo la kuhamasisha kinga na udhibiti wa magonjwa yasiyoambukiza.Aidha, timu ya mradi iliambatana na baadhi ya wanufaika wa kliniki za magonjwa yasiyoambukiza zinazotekelezwa kupitia PEN-Plus katika vituo mbalimbali vya afya nchini, ambapo walipata fursa ya kuelezea uzoefu wao kuhusu namna huduma hizo zilivyoboreshwa na kurahisisha upatikanaji wa matibabu katika maeneo yao.Ushiriki wa NIMR katika ICPPA 2026 unaonesha mchango wa taasisi katika kuimarisha huduma za magonjwa yasiyoambukiza kupitia tafiti, ushahidi wa kisayansi na utekelezaji wa mifumo bunifu ya utoaji huduma za afya inayolenga kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan walioko katika maeneo yenye uhitaji mkubwa. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR kupitia PEN-Plus Yafikisha Huduma za Magonjwa Yasiyoambukiza Karibu na Wananchi Read More »