Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Kituo cha Muhimbili, imewajengea uwezo watumishi wa afya 18 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana (Amana RRH) katika uandishi wa maandiko ya utafiti (Proposal Development), hatua inayolenga kuboresha huduma za afya kwa jamii kupitia tafiti zenye ubora na ushahidi wa kisayansi.

Mafunzo hayo ya siku nne yalifanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Januari 2026 katika hospitali hiyo yakilenga kuwawezesha watoa huduma wa afya kubuni, kuandaa na kuwasilisha mapendekezo bora ya tafiti za kisayansi zinazoweza kupata ufadhili na kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya.

Kupitia mafunzo hayo ya vitendo, washiriki walipata ujuzi wa kuandaa maandiko ya kisayansi yenye viwango, kuimarisha uwezo wa uandishi wa kitaaluma, kuelewa na kuzingatia maadili ya utafiti pamoja na kutumia takwimu sahihi katika kutatua changamoto za kiafya zinazowakabili wananchi.

Akifungua mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Bryceson Loti Kiweru, alisema utafiti ni nyenzo muhimu isiyoweza kuepukika katika sekta ya afya.

“Swala zima la utafiti haliepukiki katika sekta ya afya na inahitajika ushirikiano na taasisi zinazofanya utafiti ili kuboresha huduma za afya nchini,” alisema Dkt. Kiweru.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Idara ya Tafiti kutoka kituo cha NIMR Muhimbili, Dkt. Ester Mbutolwe, alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya takwimu katika kuibua suluhisho la changamoto za afya.

“Kila mtu akijengewa uwezo vizuri anaweza kutoa mchango wake katika kuboresha afya za wananchi. Takwimu sahihi ni msingi wa utafiti wenye matokeo ya kuaminika. Ushirikiano kati ya NIMR na hospitali za rufaa za mkoa ni muhimu,” alisisitiza Dkt. Mbutolwe.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za NIMR za kuimarisha tafiti za afya nchini kwa kuwajengea uwezo wataalamu walioko kwenye vituo vya kutolea huduma, ili tafiti zinazofanyika ziweze kutoa majibu ya changamoto halisi za jamii na kuboresha ubora wa huduma za afya nchini.

Section Title

CONGRATULATIONS

The National Institute for Medical Research (NIMR) extends its heartfelt congratulations to Dr. Nyanda Elias Ntinginya on his selection as a 2026 Kofi Annan Fellow in Global Health Leadership...

NIMR Launches DIMENSION Project to Advance Digital Innovation in Mental Health Care for People Living with HIV

NIMR Muhimbili Centre has launched DIMENSION (Digital Empowerment for Mental Health in Tanzania: Enhancing Healthcare Capacity through Innovative Digital Training Solutions for People Living with...

NIMR Receives Bioinformatics Equipment to Advance Health Research and Genomic Data Analysis

The National Institute for Medical Research (NIMR) has received bioinformatics equipment and systems from AMREF Health Africa Tanzania to advance health research and genomic data analysis, while...

NIMR YAONYESHA MATUMIZI YA UTAFITI KUBORESHA HUDUMA ZA VVU KWA MAMA NA MTOTO

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umeonesha kwamba upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua unaweza kusaidia kuwatambua mapema...

SALAMU ZA POLE

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo...

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu

Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limewataka watafiti kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika vituo vya Taasisi kuongeza machapisho na ubunifu wa utafiti, ili...

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya

Serikali imetoa wito kwa watafiti na wadau wa tiba asili kuongeza kasi ya tafiti, uthibitishaji wa kisayansi na uwekezaji katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, ili zenye ushahidi wa usalama, ubora...

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Dira 2050