Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tarehe 26 Februari 2026, kupitia mradi wa RAFT (Resilience Against Future Threats through Vector Control), imewasilisha matokeo ya utafiti kuhusu magonjwa ya mlipuko yanayoenezwa na mbu pamoja na usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu, hatua inayolenga kuimarisha ustahimilivu wa taifa katika kukabiliana na vitisho vya magonjwa hayo.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Tafiti, Dkt. Nyanda Elias Ntinginya, amesema Tanzania inahitaji kuimarisha mifumo yake ya ufuatiliaji na maandalizi ili kukabiliana kwa ufanisi na ongezeko la vitisho vya magonjwa yanayoenezwa na mbu.
Amesisitiza kuwa tafiti za kisayansi zinapaswa kuwa msingi wa maamuzi ya kisera, hasa katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya mazingira, ukuaji wa miji na ongezeko la mwingiliano wa watu vinaongeza hatari ya milipuko ya magonjwa kama dengue na magonjwa mengine ya virusi yanayoenezwa na mbu.
Kwa upande wake, Mtafiti Kiongozi wa Mradi wa RAFT, Dkt. Alphaxard Manjurano, amesema lengo la mkutano huo lilikuwa kuwasilisha matokeo muhimu kuhusu usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu na vitisho vya magonjwa ya mlipuko yanayoenezwa na mbu, pamoja na kuyajadili kwa kina na wadau wakuu wa udhibiti wa wadudu dhurifu nchini.
Akiwasilisha matokeo ya tathmini ya kitaifa ya utayari wa mfumo wa afya kukabiliana na vitisho vya mbu, Dkt. Manjurano alibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa vituo 34 vya ufuatiliaji wa malaria (sentinel sites), bado kuna haja ya kuanzisha programu mahsusi ya kitaifa ya ufuatiliaji wa kawaida wa mbu wanaoeneza magonjwa.
“Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2024, ufuatiliaji wa mbu wa kuanzia hatua za mabuu hadi mbu waliokomaa haujawahi kufanyika kwa mfumo wa kitaifa. Hii inaonesha umuhimu wa kuimarisha mfumo wa utambuzi wa mapema wa hatari za milipuko ya magonjwa ya yanayoenezwa na wadudu,” alisisitiza Dkt. Manjurano.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya kupitia Programu ya Taifa ya Udhibiti wa Malaria, Bw. Winfred Mwafongo, amesema matokeo hayo yatasaidia kuboresha sera na miongozo ya kukabiliana na malaria na magonjwa mengine yanayoenezwa na wadudu.
Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Jovin Kitau, ameipongeza NIMR kwa kufanya utafiti huo, akisema utachangia kuimarisha kinga ya jamii dhidi ya magonjwa yanayoenezwa na wadudu na kuongeza usalama wa afya ya umma.
Aidha, Mtafiti Mkuu kutoka NIMR, Dkt. William Kisinza, amesema katika majadiliano ya kikao hicho wadau wamependekeza kuimarishwa kwa programu maalumu inayosimamia masuala ya wadudu dhurifu ili kuongeza ufanisi wa udhibiti wa magonjwa yanayoenezwa na wadudu.
Kwa upande wake, Bi. Jackeline Martin, Mtafiti kutoka NIMR aliyefanya utafiti kuhusu ufanisi wa viuatilifu vilivyopo kwenye vyandarua, amesema matokeo yanaonesha ongezeko la usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu hivyo, jambo linaloonesha umuhimu wa kuendelea kuboresha mikakati ya udhibiti ili kuhakikisha vyandarua vinaendelea kuwa na ufanisi.
Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Protea, jijini Dar es Salaam, uliwakutanisha wadau mbalimbali wa udhibiti wa wadudu dhurifu kutoka Wizara ya Afya, NIMR, Shirika la Afya Duniani (WHO), Taasisi ya Afya ya Ifakara, pamoja na wadau wengine wa sekta ya afya.

Section Title

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

NIMR to Lead Ethical Oversight in a Multicountry Trial Exploring New Approaches to Prevent Childhood Diarrhoeal Diseases.

The National Institute for Medical Research (NIMR) is leading ethical oversight in a new multicountry clinical trial investigating whether probiotics can enhance the protection provided by rotavirus...

NIMR TABORA RESEARCH CENTRE A CENTURY OF SCIENCE: A NEW ERA OF PUBLIC HEALTH IMPACT

From a Sleeping Sickness Unit to a Modern Public Health Research Hub For more than a century, NIMR Tabora has connected scientific discovery with practical public health action. Established in Tabora...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

NIMR and HJF Strengthen Health Research Collaboration

The National Institute for Medical Research (NIMR) and the U.S.-based Henry M. Jackson Foundation (HJF) have discussed strategies to strengthen the existing collaboration in health research including...

NIMR and Museen Stade Strengthen Strategic Partnership to Advance Research, Heritage and Tourism at Amani Hill

The National Institute for Medical Research (NIMR) and Museen Stade of Germany have formalized their partnership through the signing of a collaboration agreement under the WAYS – Towards Fair and...

NIMR Mbeya Yawafikia Wakulima, Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utafiti wa Afya.

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Kituo cha Mbeya, imetumia Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) Kanda ya Kusini kuwafikia wananchi moja kwa moja, hususan wakulima...

Today is your last opportunity to submit your abstract for the 5th Traditional Medicine Scientific Conference.

Today is your last opportunity to submit your abstract for the 5th Traditional Medicine Scientific Conference.Share your research, engage with experts, and contribute to advancing evidence-based...

NIMR, Partners Advance Efforts to Strengthen Tanzania’s Clinical Trial Oversight Framework

The National Institute for Medical Research (NIMR) in collaboration with the Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA), other local and international partners, on 28th July, 2026...

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Dira 2050