Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za tiba asili kupitia tafiti, na uanzishwaji wa kiwanda cha kuzalisha dawa za tiba asili cha NIMR Mabibo kufuatia juhudi kubwa za Serikali kuhakikisha dawa salama na zenye ubora zinapatikana kwa wingi nchini.
Akizungumza tarehe 29 Agosti, 2025 katika Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika jijini Dodoma, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, aliipongeza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa hatua kubwa zilizopigwa katika tafiti na uhamasishaji wa matumizi ya dawa za tiba asili.
Dkt. Kazungu alisema moja ya mafanikio makubwa ya NIMR ni uanzishwaji wa kiwanda cha Mabibo cha kuzalisha dawa za tiba asili ambacho kinatumia malighafi kutoka kwa wakulima wa miti dawa. “Kiwanda hiki hakijaishia tu kuzalisha dawa salama na zenye ufanisi na ubora, bali pia kimetoa fursa za ajira kwa wananchi na kuongeza kipato kwa wakulima wa malighafi hizo,” alisisitiza Dkt Kazungu.
Aidha, alitembelea banda la NIMR katika maonesho na kupongeza jitihada zilizofanywa huku akishauri kuimarisha tafiti zinazohusu tiba asili kwa magonjwa ya figo ambayo yanaongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni.
Akitoa maelezo katika banda la NIMR Meneja wa kituo cha NIMR Mabibo Dkt. Emmanuel Peter alibainisha mchango wa NIMR katika kukuza tiba asili nchini kuwa ni pamoja na kufanya tafiti za tiba asili, kushiriki katika huduma jumuishi, kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa za tiba asili, kuhamasisha tafiti, ugunduzi na matumizi ya dawa za tiba asili, kuimarisha ushirikiano na wadau wa tiba asili
Dkt. Peter alisema Kwa sasa, wananchi wanapata huduma jumuishi za tiba asili katika hospitali za rufaa za mikoa 14 ambapo mteja anaweza kuchagua tiba ya kisasa, tiba asili au kutumia zote kwa pamoja. “Huduma hii inamuwezesha mteja kufanyiwa vipimo vya kitaalamu na kupewa ushauri sahihi kuhusu tiba inayomfaa.
Maadhimisho hayo, yenye kaulimbiu “Tuimarishe Huduma za Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi,” yalianza tarehe 25 Agosti 2025 na yanatarajiwa kutamatika tarehe 31 Agosti 2025. Tukio hili limewakutanisha wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala kutoka maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kubadilishana uzoefu, na kuhamasisha matumizi ya dawa za tiba asili kwa manufaa ya jamii.

Section Title

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

NIMR to Lead Ethical Oversight in a Multicountry Trial Exploring New Approaches to Prevent Childhood Diarrhoeal Diseases.

The National Institute for Medical Research (NIMR) is leading ethical oversight in a new multicountry clinical trial investigating whether probiotics can enhance the protection provided by rotavirus...

NIMR TABORA RESEARCH CENTRE A CENTURY OF SCIENCE: A NEW ERA OF PUBLIC HEALTH IMPACT

From a Sleeping Sickness Unit to a Modern Public Health Research Hub For more than a century, NIMR Tabora has connected scientific discovery with practical public health action. Established in Tabora...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...

NIMR and HJF Strengthen Health Research Collaboration

The National Institute for Medical Research (NIMR) and the U.S.-based Henry M. Jackson Foundation (HJF) have discussed strategies to strengthen the existing collaboration in health research including...

NIMR and Museen Stade Strengthen Strategic Partnership to Advance Research, Heritage and Tourism at Amani Hill

The National Institute for Medical Research (NIMR) and Museen Stade of Germany have formalized their partnership through the signing of a collaboration agreement under the WAYS – Towards Fair and...

NIMR Mbeya Yawafikia Wakulima, Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utafiti wa Afya.

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Kituo cha Mbeya, imetumia Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) Kanda ya Kusini kuwafikia wananchi moja kwa moja, hususan wakulima...

Today is your last opportunity to submit your abstract for the 5th Traditional Medicine Scientific Conference.

Today is your last opportunity to submit your abstract for the 5th Traditional Medicine Scientific Conference.Share your research, engage with experts, and contribute to advancing evidence-based...
Dira 2050