Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeanza rasmi utekelezaji wa utafiti wa majaribio ya tiba ya kuharakisha kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha. Hayo yamebainishwa wakati wa kuendesha mafunzo ya siku mbili ya kutekeleza utafiti kwa watafiti na watoa huduma wa afya kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, yalifunguliwa rasmi na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Mwinjuma M. Mkungu. Katika hotuba yake, aliipongeza NIMR kwa kuwa kinara wa tafiti za afya nchini na kwa kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Afya katika kuandaa tafiti zenye lengo la kumaliza kabisa magonjwa yanayosumbua jamii, hususani yale yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs).
“NIMR ni nguzo muhimu katika sekta ya afya kwa kuwa inatoa ushahidi wa kisayansi unaosaidia kupanga na kutekeleza afua bora. Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi hizo,” alisema Mhe. Mkungu.
Mafunzo hayo yamefuatiwa na kuanza kwa uchukuaji wa sampuli kwa washiriki wa utafiti katika kijiji cha Ruaha, kata ya Mnazi Mmoja, Wilaya ya Lindi. Utafiti huu wa kisayansi unalenga kulinganisha tiba tofauti za magonjwa ya matende na mabusha, hususani dawa ya “Doxycycline” na “Moxidectin + Albendazole”, dhidi ya Kingatiba iliyopo sasa ya “Ivermectin + Albendazole”.
Mtafiti Mkuu wa mradi wa utafiti kutoka NIMR, Dkt. Akili Kalinga, alisema kuwa tafiti hizi zinalenga kutafuta tiba mbadala na bora zaidi ambazo zitaweza kuharakisha kutokomeza ugonjwa huo nchini. “Tumekuwa kwenye mapambano dhidi ya matende na mabusha kwa miaka mingi. Tunategemea kuwa utafiti huu utasaidia kuondoa kabisa vikwazo vinavyosababisha maambukizi ya Ugonjwa huu kuendelea katika baadhi ya maeneo.” alisema Dkt. Kalinga.
Akizungumza wakati wa zoezi la uchukuaji wa sampuli, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruaha, Bi. Salima Kidamchong`we, alisema kuwa utafiti huo ni muhimu sana kwa jamii yao kwa sababu unawapa fursa ya kujua hali yao ya kiafya. “Tunatoa shukrani kwa NIMR na Wizara ya Afya kwa kutuletea utafiti huu. Ni jambo la maana na lenye manufaa kwa wananchi wetu,” alisema.
Naye mmoja wa washiriki wa utafiti kutoka kijiji cha Ruaha kata ya Mnazi Mmoja, Bw. Ali Bakari Natulama, aliipongeza NIMR kwa juhudi zake na kusema kwamba tafiti kama hizi zinasaidia sana katika kuelimisha jamii na kuwakinga na magonjwa hatari kama matende na mabusha.
Kwa sasa, ugonjwa wa matende na mabusha bado upo katika baadhi ya Halmashauri za wilaya nchini Tanzania ikiwemo Lindi Manispaa, Mtama, Mikindani, Kinondoni na Pangani. Licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa Halmashauri 114 kutokomeza maambukizi ya Ugonjwa na kusitisha ugawaji wa kingatiba uliofanyika kwa miaka mingi.
NIMR inatarajia kutumia matokeo ya utafiti huu kuboresha miongozo ya kitaifa na kidunia ya tiba na udhibiti wa magonjwa haya, kwa kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Afya na wadau wengine.

Section Title

CONGRATULATIONS

The National Institute for Medical Research (NIMR) extends its heartfelt congratulations to Dr. Nyanda Elias Ntinginya on his selection as a 2026 Kofi Annan Fellow in Global Health Leadership...

NIMR Launches DIMENSION Project to Advance Digital Innovation in Mental Health Care for People Living with HIV

NIMR Muhimbili Centre has launched DIMENSION (Digital Empowerment for Mental Health in Tanzania: Enhancing Healthcare Capacity through Innovative Digital Training Solutions for People Living with...

NIMR Receives Bioinformatics Equipment to Advance Health Research and Genomic Data Analysis

The National Institute for Medical Research (NIMR) has received bioinformatics equipment and systems from AMREF Health Africa Tanzania to advance health research and genomic data analysis, while...

NIMR YAONYESHA MATUMIZI YA UTAFITI KUBORESHA HUDUMA ZA VVU KWA MAMA NA MTOTO

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umeonesha kwamba upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua unaweza kusaidia kuwatambua mapema...

SALAMU ZA POLE

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo...

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu

Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limewataka watafiti kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika vituo vya Taasisi kuongeza machapisho na ubunifu wa utafiti, ili...

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya

Serikali imetoa wito kwa watafiti na wadau wa tiba asili kuongeza kasi ya tafiti, uthibitishaji wa kisayansi na uwekezaji katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, ili zenye ushahidi wa usalama, ubora...

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...
Dira 2050