Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa Kushirikiana na Wizara ya Afya, tarehe 18/08/2025 imeanza mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa maabara na watafiti kutoka taasisi mbalimbali za afya, lengo likiwa ni kuimarisha uwezo wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kuchambua (Bioinformatics) takwimu za mpangilio wa vinasaba (NGS data) za magonjwa ya mlipuko zinazozalishwa nchini Tanzania, ili kutambua aina na kufuatilia mabadiliko ya vimelea hivyo vya maradhi.
Akifungua mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mjini Morogoro, Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Epidemiolojia na Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Vida Mmbaga, amesema mafunzo hayo ni hatua muhimu katika kuimarisha uwezo wa wataalamu wa maabara kutumia teknolojia ya kisasa katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

“Kuchakata takwimu hizi kutasaidia kutoa usaidizi kwa nguzo zingine za udhibiti ambazo zinafanya kazi kwa pamoja na maabara, kwani kazi ya utabibu inategemea utambuzi kutoka maabara. Hivyo, wataalamu hawa wakiboresha uchambuzi wa kina, utaalamu wao utasaidia zaidi katika kudhibiti magonjwa,” amesema Dkt. Mmbaga.

Ameongeza kuwa Serikali inalenga kuboresha uchakataji wa takwimu za vimelea vya maradhi kwa usahihi ili kusaidia kudhibiti magonjwa kwa ufanisi na uhakika.
Naye Dkt. Clara Lubinza Mtafiti kutoka NIMR na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Global Heath Security ambao NIMR inatekeleza kwa kushirikiana na Wizara ya Afya amesema mafunzo hayo yatawasaidia wataalamu wa afya na maabara kuweza kuvisoma vinasaba vya vimelea vya magonjwa, kuvielewa ni vimelea vya aina gani na kuvitambua vinapokua vinabadilika.
Aidha Dkt. Clara ameeleza kuwa matarajio baada ya mafunzo hayo ni kuhakikisha wataalamu wa afya wanapata uwezo wa kuchambua na kutambua vimelea vinavyosababisha magonjwa mbalimbali, kubaini tabia, aina na maeneo vinaposambaa, na kutambua mapema iwapo vitabadilika. “Hatua hii itawawezesha watalaamu wetu kutoa taarifa kwa Wizara ya Afya kwa wakati, ili kuchukua hatua za haraka za kudhibiti na kuzuia usambazaji zaidi wa vimelea hivyo.” Alieleza Dkt. Clara.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na NIMR kwa kushirikiana na Wizara ya Afya yamewakutanisha pamoja wataalamu kutoa NIMR, Wizara ya Afya, Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii, Hospital ya Magonjwa ya Mlipuko Kibong`oto, na Maabara ya Afya ya Jamii ya Zanzibar.

Section Title

CONGRATULATIONS

The National Institute for Medical Research (NIMR) extends its heartfelt congratulations to Dr. Nyanda Elias Ntinginya on his selection as a 2026 Kofi Annan Fellow in Global Health Leadership...

NIMR Launches DIMENSION Project to Advance Digital Innovation in Mental Health Care for People Living with HIV

NIMR Muhimbili Centre has launched DIMENSION (Digital Empowerment for Mental Health in Tanzania: Enhancing Healthcare Capacity through Innovative Digital Training Solutions for People Living with...

NIMR Receives Bioinformatics Equipment to Advance Health Research and Genomic Data Analysis

The National Institute for Medical Research (NIMR) has received bioinformatics equipment and systems from AMREF Health Africa Tanzania to advance health research and genomic data analysis, while...

NIMR YAONYESHA MATUMIZI YA UTAFITI KUBORESHA HUDUMA ZA VVU KWA MAMA NA MTOTO

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umeonesha kwamba upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua unaweza kusaidia kuwatambua mapema...

SALAMU ZA POLE

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo...

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu

Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limewataka watafiti kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika vituo vya Taasisi kuongeza machapisho na ubunifu wa utafiti, ili...

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya

Serikali imetoa wito kwa watafiti na wadau wa tiba asili kuongeza kasi ya tafiti, uthibitishaji wa kisayansi na uwekezaji katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, ili zenye ushahidi wa usalama, ubora...

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...
Dira 2050