Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James Mdoe, leo tarehe 25 Julai 2025 amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Muhimbili, akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud.
Katika ziara hiyo, Prof. Mdoe ametembelea Maabara Kuu ya Kifua Kikuu, ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha NIMR Muhimbili na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma wa Wizara ya Afya. Maabara hiyo ni miongoni mwa nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya kifua kikuu nchini na kanda ya Afrika. Alisisitiza kuwa mwelekeo wa uongozi wake ni kuona NIMR inazidi kung’ara kitaifa na kimataifa kupitia tafiti za afya zenye athari chanya kwa jamii.
Baada ya kutembelea maabara, Prof. Mdoe alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa kituo hicho ambapo aliwatia moyo kuongeza tija na ubunifu katika kazi zao za utafiti, akisisitiza umuhimu wa kufikia malengo ambayo Taasisi imejiwekea. Aliahidi kushirikiana kwa karibu na menejimenti ya Taasisi katika kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof. Said Aboud alimpongeza Prof. Mdoe kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Baraza la NIMR.
Aidha aliwapongeza watumishi wa Kituo cha NIMR Muhimbili kwa mchango wao mkubwa katika kushiriki kutengeneza sera na miongozi ya tiba ya kifua kikuu na UKIMWI kitaifa na kimataifa kutokana na matokeo ya tafiti. Hata hivyo, aliwasihi kuongeza juhudi katika kuchapisha matokeo ya tafiti na kuandaa vijarida sera ili kuongeza ushahidi wa kisayansi kutoka katika kazi za utafiti wanazofanya. “Katika mwaka wa fedha 2024/25, tumefanikiwa kuchapisha machapisho 46 ya tafiti za afya katika majarida ya kitaifa, kikanda na kimataifa na vijarida sera 12 kutoka katika kituo cha NIMR Muhimbili. Hili ni jambo la kujivunia lakini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi,” alisema Prof. Aboud.
Ziara hiyo imeonesha dhamira ya dhati ya uongozi wa juu wa NIMR katika kuimarisha usimamizi, kuongeza uwajibikaji na kuendeleza utafiti wa afya unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Section Title

CONGRATULATIONS

The National Institute for Medical Research (NIMR) extends its heartfelt congratulations to Dr. Nyanda Elias Ntinginya on his selection as a 2026 Kofi Annan Fellow in Global Health Leadership...

NIMR Launches DIMENSION Project to Advance Digital Innovation in Mental Health Care for People Living with HIV

NIMR Muhimbili Centre has launched DIMENSION (Digital Empowerment for Mental Health in Tanzania: Enhancing Healthcare Capacity through Innovative Digital Training Solutions for People Living with...

NIMR Receives Bioinformatics Equipment to Advance Health Research and Genomic Data Analysis

The National Institute for Medical Research (NIMR) has received bioinformatics equipment and systems from AMREF Health Africa Tanzania to advance health research and genomic data analysis, while...

NIMR YAONYESHA MATUMIZI YA UTAFITI KUBORESHA HUDUMA ZA VVU KWA MAMA NA MTOTO

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umeonesha kwamba upimaji wa kiwango cha virusi vya VVU kwa mama wakati wa kujifungua unaweza kusaidia kuwatambua mapema...

SALAMU ZA POLE

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo...

Baraza la NIMR Lawataka Watafiti Kutumia Fursa Kuongeza Machapisho na Ubunifu

Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limewataka watafiti kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika vituo vya Taasisi kuongeza machapisho na ubunifu wa utafiti, ili...

Serikali Yataka Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi Kujumuishwa Katika Mfumo Rasmi wa Afya

Serikali imetoa wito kwa watafiti na wadau wa tiba asili kuongeza kasi ya tafiti, uthibitishaji wa kisayansi na uwekezaji katika uzalishaji wa dawa za tiba asili, ili zenye ushahidi wa usalama, ubora...

Prof. Mdoe Asisitiza Kukamilishwa kwa Ukarabati wa Kituo cha NIMR Tukuyu

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James E. Mdoe, amesema ataendelea kushirikiana na Menejimenti ya NIMR katika kuhakikisha maeneo yaliyobaki ya...

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya...
Dira 2050