Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe (MNMH) leo tarehe 13/02/2026 zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) inayolenga kuimarisha mashirikiano katika tafiti, mafunzo na matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma bora za afya ya akili nchini.
Kupitia ushirikiano huu, taasisi hizo zitaongeza uwezo wa wataalamu wa afya ya akili kupitia mafunzo na tafiti shirikishi zitakazotoa ushahidi wa kisayansi kwa lengo la kuboresha sera, miongozo na utoaji wa huduma kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza ufanisi na ubora kwa wananchi. Ushirikiano huo pia utahusisha utekelezaji wa pamoja wa miradi ya utafiti, kuandika machapisho ya kitaaluma, kuandaa vijarida sera na ushawishi katika kuboresha huduma kwa wananchi.
Makubaliano haya yanakusudia kupanua wigo wa tafiti katika eneo la afya ya akili, kuunganisha utaalamu, matumizi ya rasilimali watu wenye ubobezi na uzoefu wa taasisi hizo, na kuhakikisha matokeo ya tafiti yanawafikia wananchi na kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao.
Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya NIMR jijini Dodoma na kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, akiwa na Meneja wa Kituo cha NIMR Dodoma, Dk. Basiliana Emidi. Kwa upande wa MNMH, ujumbe uliongozwa na Dk. Innocent R. Mwombeki aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, akiongozana na Veronica Haule na Anewa Saweni.
Section Title
NIMR Disseminates Impactful Research Findings at the 7th Africa Continental World AMR Awareness Week
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.


