NIMR

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Kituo chake cha Muhimbili, imeendesha mafunzo maalumu ya uandishi wa andiko la kitafiti kwa watumishi wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke. Mafunzo hayo ya siku tatu, yaliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2025, yalilenga kuwajengea uwezo washiriki katika kubuni, kuandaa na kuwasilisha mapendekezo bora ya tafiti za kisayansi.
Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kufanya mazoezi kwa vitendo kuhusu hatua muhimu za uandishi wa andiko la utafiti, ikiwemo kuandaa mapendekezo yenye ubora, kuimarisha uwezo wa uandishi wa kisayansi, kuelewa na kutekeleza maadili ya utafiti, pamoja na kubadilisha mawazo ya kitaalamu na kuwa tafiti zenye matokeo chanya na zinazoweza kupata ufadhili.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Kukuza na Kuratibu Tafiti NIMR (DRCP) Dkt. Nyanda E. Ntinginya, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Temeke kwa kuthamini umuhimu wa mafunzo hayo na kuhakikisha ushiriki mpana wa watumishi wake. Amesisitiza kuwa ujuzi walioupata washiriki unapaswa kutumika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kuanzisha, kuendesha na kuchapisha tafiti zenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Dkt. Nyanda pia alibainisha kuwa NIMR itaendelea kuimarisha ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya Temeke katika kukuza uwezo wa watumishi, kuendeleza tafiti za pamoja na kuhamasisha matumizi ya ushahidi wa kisayansi katika kuboresha huduma za afya nchini.
Mafunzo hayo yanaibua matumaini mapya kwa watumishi wa afya Temeke, huku yakitarajiwa kuongeza ubunifu, ushindani na tija katika uandaaji wa tafiti zenye mchango mkubwa katika mfumo wa afya wa Tanzania.

Section Title

Wanawake wa NIMR Mbeya Watoa Zawadi kwa Kliniki za Utafiti wa Afya Kusaidia Washiriki

Wanawake wa Kituo cha Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Mbeya wametoa zawadi za mashuka kwa kliniki za utafiti zinazotumiwa na kituo hicho ili kusaidia washiriki wa tafiti...

NIMR Yafanya Mkutano wa 17 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Yajadili Mpango Mkakati wa 2026–2031 na Bajeti ya 2026/2027

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo tarehe 21 Aprili 2026, imefanya Mkutano wa 17 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper jijini Dodoma, ukiwa...

NIMR Strengthens International Collaboration in Tuberculosis and Diabetes Mellitus Research at PROTID Annual General Meeting

The National Institute for Medical Research (NIMR) has continued to emphasize the importance of international collaboration in advancing research, training, and innovation aimed at addressing the...

NIMR Director General Honored for Outstanding Contributions to Advancing Medical Science, Research and Capacity Building

The Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), Prof. Said S. Aboud, has been honoured with the African Excellence and Personality Award (AEPA 2026) in Medical Science...

NIMR Scientists Ranked Among Tanzania Top 50 by the AD Scientific Index 2026

The National Institute for Medical Research (NIMR) has once again demonstrated its leadership in scientific research with five of its distinguished scientists ranked among the Top 50 scientists in...

Decade-Long Research Led by NIMR Shapes Africa’s Push for Integrated HIV and NCD Care

New evidence from a decade of research led by Tanzania’s National Institute for Medical Research (NIMR) on integrated HIV and non-communicable disease (NCD) care is driving renewed efforts across...

Watumishi NIMR Wapatiwa Mafunzo ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Rushwa Mahali pa Kazi na Afya ya Akili

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendelea kuonesha dhamira yake ya kujenga watumishi wenye weledi, uadilifu, uwajibikaji na afya njema kwa kuendesha mafunzo maalumu...

NIMR Researchers Shine with DZIF Early Career Scientists Grant

Researchers from the National Institute for Medical Research (NIMR), Mbeya Centre, have earned international recognition after five early career scientists were awarded the prestigious Deutsches...

NIMR Yasisitiza Tafiti Zinazotatua Changamoto za Afya Katika Maandalizi ya Bajeti ya 2026/2027

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said Aboud, ameitaka taasisi hiyo kuimarisha uwezo wake wa kifedha na kuwekeza katika tafiti zinazolenga kutatua...

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.