Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Kituo chake cha Muhimbili, imeendesha mafunzo maalumu ya uandishi wa andiko la kitafiti kwa watumishi wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke. Mafunzo hayo ya siku tatu, yaliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2025, yalilenga kuwajengea uwezo washiriki katika kubuni, kuandaa na kuwasilisha mapendekezo bora ya tafiti za kisayansi.
Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kufanya mazoezi kwa vitendo kuhusu hatua muhimu za uandishi wa andiko la utafiti, ikiwemo kuandaa mapendekezo yenye ubora, kuimarisha uwezo wa uandishi wa kisayansi, kuelewa na kutekeleza maadili ya utafiti, pamoja na kubadilisha mawazo ya kitaalamu na kuwa tafiti zenye matokeo chanya na zinazoweza kupata ufadhili.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Kukuza na Kuratibu Tafiti NIMR (DRCP) Dkt. Nyanda E. Ntinginya, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Temeke kwa kuthamini umuhimu wa mafunzo hayo na kuhakikisha ushiriki mpana wa watumishi wake. Amesisitiza kuwa ujuzi walioupata washiriki unapaswa kutumika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kuanzisha, kuendesha na kuchapisha tafiti zenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Dkt. Nyanda pia alibainisha kuwa NIMR itaendelea kuimarisha ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya Temeke katika kukuza uwezo wa watumishi, kuendeleza tafiti za pamoja na kuhamasisha matumizi ya ushahidi wa kisayansi katika kuboresha huduma za afya nchini.
Mafunzo hayo yanaibua matumaini mapya kwa watumishi wa afya Temeke, huku yakitarajiwa kuongeza ubunifu, ushindani na tija katika uandaaji wa tafiti zenye mchango mkubwa katika mfumo wa afya wa Tanzania.
Section Title
NIMR Disseminates Impactful Research Findings at the 7th Africa Continental World AMR Awareness Week
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.




