Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Apongeza Kituo cha Utafiti wa Dawa za Tiba Asili Mabibo
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James Mdoe, amefurahishwa na kazi inayofanywa na Kituo cha Utafiti wa Dawa za Tiba Asili cha NIMR Mabibo katika kuendeleza tafiti za tiba mbadala kwa afya ya Watanzania.Pongezi hizo alizitoa tarehe 24 Juni, 2025 alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo. Prof. Mdoe alitembelea kituo hicho kwa ajili ya kujitambulisha na kuona maendeleo ya tafiti, ugunduzi na uzalishaji wa tiba asili.Akimkaribisha katika kituo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud alimpongeza Prof. James Mdoe kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi na kumuahidi kumpa ushirikiano ili kufanikisha malengo ya Taasisi. Aliwasilisha taarifa ya kituo iliyoeleza mafanikio mbalimbali katika maeneo ya rasilimali watu, vitendea kazi, miundombinu ya majengo na maabara pamoja na maendeleo ya uzalishaji ya dawa za tiba asili. Akizungumza na watumishi wa kituo hicho, Mwenyekiti wa Baraza alielekeza Taasisi kuandaa mpango mkakati wa kutofautisha huduma na biashara, watafiti kuongeza machapisho ya tafiti, kusajili haki miliki, kuongeza ushirikiano na taasisi nyingine za tiba asili kama ITM na watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha malengo ya Taasisi.Prof. Mdoe alisisitiza kuwa tiba asili ni hazina muhimu inayoweza kutoa suluhisho la changamoto nyingi za kiafya na akahimiza juhudi zaidi katika kukuza ubunifu na utafiti katika eneo hilo. Pia alishukuru kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi katika kuhakikisha kituo kinapiga hatua zaidi. Section Title Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Apongeza Kituo cha Utafiti wa Dawa za Tiba Asili Mabibo ByErick Mboma July 25, 2025 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeanza rasmi utekelezaji wa utafiti wa majaribio ya tiba ya kuharakisha kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha. Hayo… Read More NIMR Yaanza Utekelezaji wa Utafiti wa Majaribio ya Dawa Kutokomeza Maambukizi ya Ugonjwa wa Matende na Mabusha Lindi na Mtwara ByErick Mboma July 16, 2025 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeanza rasmi utekelezaji wa utafiti wa majaribio ya tiba ya kuharakisha kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha. Hayo… Read More NIMR Yawanoa Watafiti Vijana Kuandika Maandiko ya Tafiti za Afya Yanayoweza Kushindana Kimataifa ByErick Mboma July 1, 2025 Uncategorized aasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendesha mafunzo maalumu kwa watafiti vijana 13 kuhusu namna ya kuandaa maandiko ya tafiti za afya kwa madhumuni ya kuvutia washirika wa… Read More NIMR Amani Centre Passes OECD GLP Surveillance Inspection, Reaffirms Position as Leading Public Test Facility in East Africa ByErick Mboma June 30, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) Amani Research Centre has completed a rigorous annual surveillance and inspection by the South African National Accreditation System (SANAS)… Read More Kamishna Jenerali wa DCEA Aipongeza NIMR kwa Kuunga Mkono Juhudi za Serikali za Kupiga Vita Dawa za Kulevya ByErick Mboma June 27, 2025 Uncategorized Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Aretas Lyimo ameipongeza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kuunga mkono mapambano… Read More NIMR Advocates for Broader One Health Strategy at Regional Health Conference in Juba ByErick Mboma June 26, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) has called for a bold expansion of the One Health approach to address both communicable and non communicable diseases (NCDs) in Africa during the… Read More Mkurugenzi Mkuu NIMR Atoa Wito wa Uadilifu kwa Watumishi wa Umma ByErick Mboma June 23, 2025 Uncategorized Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Said Aboud, amewapongeza watumishi wa NIMR kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, uwajibikaji na uadilifu. Vilevile… Read More NIMR Yadhamiria Kuiboresha Tabora kuwa Kitovu cha Utafiti wa Afya Kanda ya Magharibi Mwa Tanzania ByErick Mboma June 22, 2025 Uncategorized Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Said Aboud, tarehe 21 Juni 2025, amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Tabora, kwa lengo la… Read More Eswatini Delegation Commends NIMR Ethical Oversight in Health Research ByErick Mboma June 21, 2025 Uncategorized A delegation from the Eswatini Health and Human Research Review Board (EHHRB) has commended National Institute for Medical Research (NIMR) for its robust ethical review and approval systems in health… Read More