Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Aonyesha Dhamira ya Kuimarisha Utafiti wa Afya
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James Mdoe, leo tarehe 25 Julai 2025 amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Muhimbili, akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud.Katika ziara hiyo, Prof. Mdoe ametembelea Maabara Kuu ya Kifua Kikuu, ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha NIMR Muhimbili na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma wa Wizara ya Afya. Maabara hiyo ni miongoni mwa nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya kifua kikuu nchini na kanda ya Afrika. Alisisitiza kuwa mwelekeo wa uongozi wake ni kuona NIMR inazidi kung’ara kitaifa na kimataifa kupitia tafiti za afya zenye athari chanya kwa jamii. Baada ya kutembelea maabara, Prof. Mdoe alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa kituo hicho ambapo aliwatia moyo kuongeza tija na ubunifu katika kazi zao za utafiti, akisisitiza umuhimu wa kufikia malengo ambayo Taasisi imejiwekea. Aliahidi kushirikiana kwa karibu na menejimenti ya Taasisi katika kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa.Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof. Said Aboud alimpongeza Prof. Mdoe kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Baraza la NIMR.Aidha aliwapongeza watumishi wa Kituo cha NIMR Muhimbili kwa mchango wao mkubwa katika kushiriki kutengeneza sera na miongozi ya tiba ya kifua kikuu na UKIMWI kitaifa na kimataifa kutokana na matokeo ya tafiti. Hata hivyo, aliwasihi kuongeza juhudi katika kuchapisha matokeo ya tafiti na kuandaa vijarida sera ili kuongeza ushahidi wa kisayansi kutoka katika kazi za utafiti wanazofanya. “Katika mwaka wa fedha 2024/25, tumefanikiwa kuchapisha machapisho 46 ya tafiti za afya katika majarida ya kitaifa, kikanda na kimataifa na vijarida sera 12 kutoka katika kituo cha NIMR Muhimbili. Hili ni jambo la kujivunia lakini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi,” alisema Prof. Aboud.Ziara hiyo imeonesha dhamira ya dhati ya uongozi wa juu wa NIMR katika kuimarisha usimamizi, kuongeza uwajibikaji na kuendeleza utafiti wa afya unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania. Section Title Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Aonyesha Dhamira ya Kuimarisha Utafiti wa Afya ByErick Mboma July 26, 2025 Uncategorized Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James Mdoe, amefurahishwa na kazi inayofanywa na Kituo cha Utafiti wa Dawa za Tiba Asili cha NIMR Mabibo katika… Read More Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Apongeza Kituo cha Utafiti wa Dawa za Tiba Asili Mabibo ByErick Mboma July 25, 2025 Uncategorized Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James Mdoe, amefurahishwa na kazi inayofanywa na Kituo cha Utafiti wa Dawa za Tiba Asili cha NIMR Mabibo katika… Read More NIMR Yaanza Utekelezaji wa Utafiti wa Majaribio ya Dawa Kutokomeza Maambukizi ya Ugonjwa wa Matende na Mabusha Lindi na Mtwara ByErick Mboma July 16, 2025 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeanza rasmi utekelezaji wa utafiti wa majaribio ya tiba ya kuharakisha kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha. Hayo… Read More NIMR Yawanoa Watafiti Vijana Kuandika Maandiko ya Tafiti za Afya Yanayoweza Kushindana Kimataifa ByErick Mboma July 1, 2025 Uncategorized aasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendesha mafunzo maalumu kwa watafiti vijana 13 kuhusu namna ya kuandaa maandiko ya tafiti za afya kwa madhumuni ya kuvutia washirika wa… Read More NIMR Amani Centre Passes OECD GLP Surveillance Inspection, Reaffirms Position as Leading Public Test Facility in East Africa ByErick Mboma June 30, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) Amani Research Centre has completed a rigorous annual surveillance and inspection by the South African National Accreditation System (SANAS)… Read More Kamishna Jenerali wa DCEA Aipongeza NIMR kwa Kuunga Mkono Juhudi za Serikali za Kupiga Vita Dawa za Kulevya ByErick Mboma June 27, 2025 Uncategorized Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Aretas Lyimo ameipongeza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kuunga mkono mapambano… Read More NIMR Advocates for Broader One Health Strategy at Regional Health Conference in Juba ByErick Mboma June 26, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) has called for a bold expansion of the One Health approach to address both communicable and non communicable diseases (NCDs) in Africa during the… Read More Mkurugenzi Mkuu NIMR Atoa Wito wa Uadilifu kwa Watumishi wa Umma ByErick Mboma June 23, 2025 Uncategorized Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Said Aboud, amewapongeza watumishi wa NIMR kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, uwajibikaji na uadilifu. Vilevile… Read More NIMR Yadhamiria Kuiboresha Tabora kuwa Kitovu cha Utafiti wa Afya Kanda ya Magharibi Mwa Tanzania ByErick Mboma June 22, 2025 Uncategorized Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Said Aboud, tarehe 21 Juni 2025, amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Tabora, kwa lengo la… Read More
Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Aonyesha Dhamira ya Kuimarisha Utafiti wa Afya Read More »










