NIMR

Wizara ya Afya leo tarehe 26/09/2025 imezindua Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), hatua muhimu inayolenga kuimarisha utafiti wa kisayansi, kukuza ubunifu na kuhakikisha mafanikio ya Taasisi kwa ustawi wa watanzania.
Akizindua Baraza hilo katika ofisi ndogo za NIMR Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, amesisitiza umuhimu wa Baraza kutoa ushauri wa kitaalamu, kusimamia utendaji wa NIMR, na kuhakikisha matokeo ya tafiti yanachangia kuboresha huduma za afya nchini.
Aidha Dkt. Shekalaghe amesisitiza kuwa ushirikiano baina ya Baraza, Menejimenti na Wizara ya Afya ni muhimu ili kuimarisha tafiti za afya na kuhakikisha matokeo yanatumiwa ipasavyo katika kutatua changamoto za kiafya za wananchi.
Akimkaribisha Katibu Mkuu kuzindua Baraza, Mwenyekiti wa Baraza jipya Prof. James Mdoe, ameahidi kuliongoza Baraza kwa weledi na uadilifu, akisisitiza kuwa litahakikisha NIMR inatoa ushauri sahihi kwa Serikali. Amesema pia Taasisi itatumia teknolojia za kisasa na fursa za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolution) kuongeza tija katika shughuli za utafiti.
โ€œMheshimiwa Katibu MkuuTunapenda kukuhakikishia kuwa, tupo tayari kwa kazi. Tutaweka juhudi zaidi na maarifa katika kutoa mchango wetu wa ushauri kwa mapana zaidi ili Taasisi iendelee kufanya kazi zake kwa ubora zaidi siku hadi siku ili kufikia malengo yake kwa faida ya Watanzaniaโ€. Amesisitiza Prof. Mdoe
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, aliwasilisha mafanikio ya Taasisi kwa kipindi cha miaka mitatu (2022/23 hadi 2024/25), akibainisha kuwa NIMR imeongeza idadi ya Miradi ya Utafiti na kufikia 150, huku machapisho ya kisayansi yameongezeka hadi 220 kwa mwaka. Aidha, vijarida sera vimefika 40 kwa mwaka lengo likiwa ni kutumika na watunga sera na wafanya maamuzi ili kuboresha huduma za afya nchini.
Prof. Aboud pia alibainisha mafanikio katika ubunifu wa tiba ikiwemo ugunduzi na uendelezaji wa broadly neutralizing antibodies (bNab) katika kituo cha NIMR Mbeya kwa ajili ya tiba ya VVU na UKIMWI. Taasisi pia imeboresha utoaji wa vibali vya utafiti na kupunguza muda kutoka miezi mitatu hadi ndani ya mwezi mmoja, kukarabati majengo chakavu ya vituo vya Gonja (Same), Amani Hill (Muheza), Ngongongare (Arusha) na Tabora, kukamilisha kusimika mitambo ya uzalishaji katika kituo cha tiba asili NIMR Mabibo, kupata ithibati ya kimataifa ya majaribio nasibu katika dawa za wadudu dhurifu (Efficacy Studies on Insecticidal Products) toka SANAS katika maabara ya NIMR Amani (Muheza), kuongezeka kwa makusanyo kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na bajeti ya Taasisi kukua kutoka Sh. bilioni 51.5 hadi Sh. bilioni 89.7 bilioni huku ikiongeza rasilimali za ndani kwa ajili ya uendeshaji wa vituo vyake.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti mpya wa Baraza, wajumbe wapya, Menejimenti ya NIMR pamoja na mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina. Hatua hizi inachagiza umuhimu wa kuendelea kufanya mageuzi ya Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1979.

Section Title

NIMR Leads Global Effort to Combat Arboviral Diseases Using One Health Approach

In demonstration of leadership in global health research, the National Institute for Medical Research (NIMR) conducted a five-day Arboviral Workshop at NIMR Mbeya Medical Research Centre under the...

Baraza Jipya la NIMR Lapatiwa Mafunzo ya Uongozi na Utawala Bora kwa Taasisi za Umma

Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limepatiwa mafunzo ya uongozi na utawala bora siku tatu kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba 2025 na Taasisi ya Uongozi (Uongozi...

NIMR Strengthens Global Research Collaboration

The National Institute for Medical Research (NIMR) on 29th September 2025, launched a five-day research collaboration meeting at Mwanza Medical Research Centre, focusing on sharing research findings...

Wizara ya Afya Yazindua Baraza la Nimr Jipya

Wizara ya Afya leo tarehe 26/09/2025 imezindua Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), hatua muhimu inayolenga kuimarisha utafiti wa kisayansi, kukuza ubunifu na...

CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM

Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section...

NIMR Yapongezwa kwa Mchango Mkubwa Katika Kukuza Tiba Asili

Wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za tiba asili kupitia tafiti, na uanzishwaji wa kiwanda cha kuzalisha dawa za tiba asili cha NIMR Mabibo kufuatia juhudi kubwa za Serikali kuhakikisha dawa...

Tiba Asili Yazidi Kungโ€™ara: Tafiti Zaidi Zahitajika

Imeelezwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza tafiti za tiba asili na kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuzalisha dawa za tiba hizo nchini, ili kuongeza tija katika kuboresha huduma za afya kwa...

Tanzania to Learn on Traditional Medicine Sector from South Korea

The Ministry of Health and the National Institute for Medical Research (NIMR) together with partner institutions embarked on a study visit to the National Institute for Korean Medicine Development...

Ministry of Health, NIMR Visits South Korea to Strengthen Innovation and Product Development in Traditional Medicine

๐— ๐—ถ๐—ป๐—ถ๐˜€๐˜๐—ฟ๐˜† ๐—ผ๐—ณ ๐—›๐—ฒ๐—ฎ๐—น๐˜๐—ต, ๐—ก๐—œ๐— ๐—ฅ ๐—ฉ๐—ถ๐˜€๐—ถ๐˜ ๐—ฆ๐—ผ๐˜‚๐˜๐—ต ๐—ž๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ๐—ฎ ๐˜๐—ผ ๐—ฆ๐˜๐—ฟ๐—ฒ๐—ป๐—ด๐˜๐—ต๐—ฒ๐—ป ๐—œ๐—ป๐—ป๐—ผ๐˜ƒ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ผ๐—ป ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ ๐—ฃ๐—ฟ๐—ผ๐—ฑ๐˜‚๐—ฐ๐˜ ๐——๐—ฒ๐˜ƒ๐—ฒ๐—น๐—ผ๐—ฝ๐—บ๐—ฒ๐—ป๐˜ ๐—ถ๐—ป ๐—ง๐—ฟ๐—ฎ๐—ฑ๐—ถ๐˜๐—ถ๐—ผ๐—ป๐—ฎ๐—น ๐— ๐—ฒ๐—ฑ๐—ถ๐—ฐ๐—ถ๐—ป๐—ฒ The Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), Prof...

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.