NIMR

Imeelezwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza tafiti za tiba asili na kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuzalisha dawa za tiba hizo nchini, ili kuongeza tija katika kuboresha huduma za afya kwa jamii. Kwa sasa, wananchi wengi wameonyesha mwamko mkubwa wa kutumia dawa za tiba asili.
Kauli hiyo imetolewa leo, Agosti 29, 2025 na Dkt. Ahmad Mohamed Makuwani Mkurugenzi wa Huduma ya Afya ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Watoto kutoka Wizara ya Afya, alipomuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika Kongamano la Nne la Kisayansi la Tiba Asili lililoandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar, jijini Dodoma.
Dkt. Makuani amewataka watafiti na wadau wa tiba asili kuwekeza nguvu katika kupata ushahidi wa kisayansi wa dawa hizo utakaosaidia kuimarisha sera za afya na kukuza ushirikiano kati ya wanasayansi na wataalamu wa tiba asili.
โ€œIli kuendeleza usawa wa afya, ni lazima dawa za tiba asili ambazo zimethibitishwa kuwa salama, zenye ufanisi na ubora ziingizwe rasmi kwenye mifumo ya utoaji huduma za afya. Tanzania tayari imeweka msingi imara kupitia Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya NIMR ya mwaka 1980,โ€ amesisitiza Dkt. Makuani.
Aidha, amependekeza kuundwa kwa mifumo ya ushirikiano na rufaa kati ya tiba asili na tiba za kisasa, kujumuisha tiba asili katika miongozo ya matibabu, na kujenga uaminifu kati ya wataalamu wa afya na waganga wa tiba asili.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, amesema taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama, ufanisi na ubora wa dawa za tiba asili, ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa zisizo salama.
Prof. Aboud amewataka waganga na wataalamu wa tiba asili kupeleka dawa zao NIMR na katika taasisi zingine zenye mamlaka ili zipimwe na kuthibitishwa. โ€œHii itawezesha dawa hizo kuwa sehemu ya huduma jumuishi katika hospitali 14 za rufaa nchini,โ€ amesisitiza Prof. Aboud.
Kongamano hilo la siku moja limewakutanisha wadau wa tiba asili kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo walijadili matokeo ya tafiti mbalimbali. Kongamano hilo pia limeambatana na Maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika, yaliyofunguliwa

Section Title

NIMR Leads Global Effort to Combat Arboviral Diseases Using One Health Approach

In demonstration of leadership in global health research, the National Institute for Medical Research (NIMR) conducted a five-day Arboviral Workshop at NIMR Mbeya Medical Research Centre under the...

Baraza Jipya la NIMR Lapatiwa Mafunzo ya Uongozi na Utawala Bora kwa Taasisi za Umma

Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limepatiwa mafunzo ya uongozi na utawala bora siku tatu kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba 2025 na Taasisi ya Uongozi (Uongozi...

NIMR Strengthens Global Research Collaboration

The National Institute for Medical Research (NIMR) on 29th September 2025, launched a five-day research collaboration meeting at Mwanza Medical Research Centre, focusing on sharing research findings...

Wizara ya Afya Yazindua Baraza la Nimr Jipya

Wizara ya Afya leo tarehe 26/09/2025 imezindua Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), hatua muhimu inayolenga kuimarisha utafiti wa kisayansi, kukuza ubunifu na...

CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM

Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section...

NIMR Yapongezwa kwa Mchango Mkubwa Katika Kukuza Tiba Asili

Wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za tiba asili kupitia tafiti, na uanzishwaji wa kiwanda cha kuzalisha dawa za tiba asili cha NIMR Mabibo kufuatia juhudi kubwa za Serikali kuhakikisha dawa...

Tiba Asili Yazidi Kungโ€™ara: Tafiti Zaidi Zahitajika

Imeelezwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza tafiti za tiba asili na kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuzalisha dawa za tiba hizo nchini, ili kuongeza tija katika kuboresha huduma za afya kwa...

Tanzania to Learn on Traditional Medicine Sector from South Korea

The Ministry of Health and the National Institute for Medical Research (NIMR) together with partner institutions embarked on a study visit to the National Institute for Korean Medicine Development...

Ministry of Health, NIMR Visits South Korea to Strengthen Innovation and Product Development in Traditional Medicine

๐— ๐—ถ๐—ป๐—ถ๐˜€๐˜๐—ฟ๐˜† ๐—ผ๐—ณ ๐—›๐—ฒ๐—ฎ๐—น๐˜๐—ต, ๐—ก๐—œ๐— ๐—ฅ ๐—ฉ๐—ถ๐˜€๐—ถ๐˜ ๐—ฆ๐—ผ๐˜‚๐˜๐—ต ๐—ž๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ๐—ฎ ๐˜๐—ผ ๐—ฆ๐˜๐—ฟ๐—ฒ๐—ป๐—ด๐˜๐—ต๐—ฒ๐—ป ๐—œ๐—ป๐—ป๐—ผ๐˜ƒ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ผ๐—ป ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ ๐—ฃ๐—ฟ๐—ผ๐—ฑ๐˜‚๐—ฐ๐˜ ๐——๐—ฒ๐˜ƒ๐—ฒ๐—น๐—ผ๐—ฝ๐—บ๐—ฒ๐—ป๐˜ ๐—ถ๐—ป ๐—ง๐—ฟ๐—ฎ๐—ฑ๐—ถ๐˜๐—ถ๐—ผ๐—ป๐—ฎ๐—น ๐— ๐—ฒ๐—ฑ๐—ถ๐—ฐ๐—ถ๐—ป๐—ฒ The Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), Prof...