Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) limepatiwa mafunzo ya uongozi na utawala bora siku tatu kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba 2025 na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute). Mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba 2025.
Mafunzo haya yamelenga kuwaongezea wajumbe wa Baraza la Taasisi uelewa kuhusu majukumu yao katika kusimamia taasisi za umma kwa ufanisi, uwajibikaji na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na matumizi sahihi ya rasilimali za umma. Maeneo muhimu ambayo
washiriki pia walijifunza ni pamoja na mbinu za Kuimarisha ufanisi wa Baraza, utawala bora na utekelezaji wa majukumu ya Baraza ambapo walipata uelewa kuhusu dhana ya uongozi wenye matokeo na uhusiano kati ya Baraza na menejimenti.
Aidha wamejifunza kuhusu mikakati madhubuti ya kudhibiti vihatarishi ndani ya taasisi, uelewa wa mambo ya rasilimali fedha, ukaguzi, manunuzi ya umma na usimamizi wa rasilimali za umma na kuweka msisitizo katika matumizi bora ya kimkakati na yenye tija kwa manufaa ya wananchi.
Kupitia ushiriki wa NIMR, mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Baraza likiwa na kazi muhimu ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya taasisi ili kuhakikisha matokeo ya tafiti yanachangia katika kuboresha sera, huduma za afya na ustawi wa jamii.
Section Title
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.
