Imeelezwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza tafiti za tiba asili na kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuzalisha dawa za tiba hizo nchini, ili kuongeza tija katika kuboresha huduma za afya kwa jamii. Kwa sasa, wananchi wengi wameonyesha mwamko mkubwa wa kutumia dawa za tiba asili.
Kauli hiyo imetolewa leo, Agosti 29, 2025 na Dkt. Ahmad Mohamed Makuwani Mkurugenzi wa Huduma ya Afya ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Watoto kutoka Wizara ya Afya, alipomuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika Kongamano la Nne la Kisayansi la Tiba Asili lililoandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar, jijini Dodoma.
Dkt. Makuani amewataka watafiti na wadau wa tiba asili kuwekeza nguvu katika kupata ushahidi wa kisayansi wa dawa hizo utakaosaidia kuimarisha sera za afya na kukuza ushirikiano kati ya wanasayansi na wataalamu wa tiba asili.
โIli kuendeleza usawa wa afya, ni lazima dawa za tiba asili ambazo zimethibitishwa kuwa salama, zenye ufanisi na ubora ziingizwe rasmi kwenye mifumo ya utoaji huduma za afya. Tanzania tayari imeweka msingi imara kupitia Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya NIMR ya mwaka 1980,โ amesisitiza Dkt. Makuani.
Aidha, amependekeza kuundwa kwa mifumo ya ushirikiano na rufaa kati ya tiba asili na tiba za kisasa, kujumuisha tiba asili katika miongozo ya matibabu, na kujenga uaminifu kati ya wataalamu wa afya na waganga wa tiba asili.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, amesema taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama, ufanisi na ubora wa dawa za tiba asili, ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa zisizo salama.
Prof. Aboud amewataka waganga na wataalamu wa tiba asili kupeleka dawa zao NIMR na katika taasisi zingine zenye mamlaka ili zipimwe na kuthibitishwa. โHii itawezesha dawa hizo kuwa sehemu ya huduma jumuishi katika hospitali 14 za rufaa nchini,โ amesisitiza Prof. Aboud.
Kongamano hilo la siku moja limewakutanisha wadau wa tiba asili kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo walijadili matokeo ya tafiti mbalimbali. Kongamano hilo pia limeambatana na Maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika, yaliyofunguliwa