Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendelea kung’ara kimataifa iliposhiriki katika kongamano la kisayansi la American Society of Tropical Medicine and Hygiene (ASTMH) kwa mwaka 2025.
Katika kongamano hilo, watafiti kadhaa wa NIMR walishiriki na kuwasilisha jumla ya tafiti 16 za kisayansi 13 zikiwa posters na 3 ni mawasilisho kwa njia ya mdomo yanayohusu tafiti bunifu katika eneo la magonjwa ya tropiki. Uwakilishi huu umeonesha ubora na thamani ya tafiti za NIMR, pamoja na mchango wake katika kuzalisha ushahidi wa kisayansi unaosaidia kuendeleza afya ya jamii duniani.
Katika hatua ya kujivunia, Bi. Catherine Bakari Mvaa ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Basel nchini Uswisi aliyefadhiliwa na mradi wa utafiti wa MSMT awamu ya kwanza wa NIMR alipokea tuzo ya Professor Dominic Kwiatkowski Fellowship ya Gates Foundation kutokana na ubora wa utafiti wake ikionyesha kutambuliwa kwa mchango wake katika maendeleo ya kisayansi.
Kongamano hili ni jukwaa la kimataifa linalowakutanisha wanasayansi na wataalamu mbalimbali kujadiliana maendeleo ya kisayansi na kitabibu katika tiba ya magonjwa ya kitropiki. Kwa mwaka huu, kongamano hilo la siku tano limefanyika jijini Toronto, Canada kuanzia tarehe 9–13 Novemba 2025.
Section Title
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.



