NIMR

Johari Buliro

NIMR to Update the National Health Research Agenda

The National Institute for Medical Research (NIMR) held on 10th April 2025 a stakeholders’ workshop at its Sub-office in Dar es Salaam aimed at updating Tanzania’s health research agenda. The workshop sought to expand the scope of the agenda by incorporating emerging priority areas including mental health, rehabilitation services, nutrition, geriatric care and the intersection between climate change and health.The event brought together key stakeholders from a wide range of institutions including representatives from the Ministry of Health specifically from the Directorate of Reseach, Planning and Innovation, Departments focusing on rehabilitation, mental health and nutrition services – Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI), Hubert Kairuki Memorial University (HKMU), Ifakara Health Institute (IHI), the Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH), Rehabilitation Organizations and NIMR researchers. These participants contributed their expertise to ensure the updated agenda reflects current health priorities, national development goals, Health Sector Strategic Plan (HSSP) V and Vision 2050.The workshop was officially opened by NIMR Director General Prof. Said Aboud and was coordinated by Dr. Nyanda Ntinginya, NIMR Director of Research Coordination and Promotion. Dr. Elizabeth Shayo served as the Secretary to the workshop while Mr. Emanuel Makundi facilitated the discussions. The outcomes of this collaborative engagement are expected to strengthen evidence-based policymaking and guide future research to improve health outcomes across the country.

NIMR to Update the National Health Research Agenda Read More »

Waziri wa Afya Aagiza NIMR Kuongeza Dawa za Tiba Asili Katika Huduma Jumuishi

Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, ameielekeza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuongeza idadi ya dawa za tiba asili zinazozalishwa na Kituo cha Utafiti cha NIMR Mabibo, ambazo utafiti wake umekamilika, ili zitumike katika huduma jumuishi zinazotolewa katika hospitali za rufaa za mkoa sita zaidi mbali na saba za sasa ili kuongeza huduma na kuisaidia jamii katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali.Mhe. Mhagama ameyasema hayo leo terehe 08/04/2025 alipotembelea banda la NIMR katika kilele cha maonesho ya Wiki ya Afya  yaliyofanyika katika viwanja vya JKCC – Dodoma. Aidha, aliipongeza NIMR kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika utafiti wa afya, zinazolenga kutatua changamoto za kiafya kwa wananchi.Aidha akieleza kuhusu mafanikio ya Tafiti, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof. Said Aboud alieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia tafiti za tiba asili zilizofanywa na taasisi hiyo. Alisema kuwa mpaka sasa, NIMR kupitia kituo chake cha Mabibo kimeweza kufanya tafiti za tiba asili ambazo zimeonyesha matokeo chanya na baadhi ya dawa zimeingizwa katika mpango wa huduma jumuishi.Prof. Aboud amesema miongoni mwa dawa zilizofanyiwa utafiti ni pamoja PERSIVIN inayotibu tezi dume, WARBUGISTAT (Magonjwa nyemelezi), NIMREGENIN (Saratani), TANGESHA (Seli mundu), TMS 2001 (Malaria) na NIMRCAF (UVIKO-19) ambayo inaendelea kusaidia jamii kutibu magojwa ya mfumo wa upumuaji. Prof. Aboud amesema NIMR katika tafiti zake za hivi karibuni imefanikiwa kuja na njia mpya ya kugundua kifua Kikuu kwa njia ya kutumia sampuli za choo na damu pamoja na kupunguza dozi kwa wagonjwa wa kifua kikuu kutoka miezi 6 ya sasa hadi 4, kupunguza dozi ya chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kutoka dozi mbili hadi moja ambayo imerahisisha utoaji huduma na kupunguza gharama kwa Serikali.    “Kwa sasa mfumo wa kidijitali wa kuombea vibali vya tafiti za afya wa National Research Information Management System (NREIMS) umeimarishwa na unasomana na mfumo wa GePG katika kufanya malipo na TMDA katika tafiti za majaribio ya kitabibu yaani ‘Clinical Trials’. Pia mfumo huu unaweza kutoa vibali kwa njia ya kidijitali na hivyo kupunguza muda wa watafiti kupata vibali vya tafiti na ruhusa ya kuchapisha matokeo ya utafiti katika majarida ya kisayansi pale wanapoomba”. Amesema Prof. Aboud Katika Wiki ya Afya, Taasisi pia ilitoa wasilisho la matokeo ya utafiti wa nchi nzima wa hali ya magonjwa yasiyoambukiza. Taarifa ambayo imetoa tathmini ya hali ya magonjwa yasioambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, figo, afya ya kinywa na meno na afya ya akili.Akimshukuru Mhe. Waziri Prof. Aboud amesema kuwa NIMR iko tayari kufanya tafiti zaidi na kuongeza bidhaa za tiba asili katika huduma jumuishi ili kuendelea kuwasaidia watanzania kukabiliana na changamoto za kiafyaMaonesho hayo ya Wiki ya Afya yameandaliwa na Wizara ya Afya yakiwakutanisha pamoja wadau mbalimbali na Taasisi za Afya kwa ajili ya kujadili na kutathimini mafanikio na maendeleo ya afya nchini.

Waziri wa Afya Aagiza NIMR Kuongeza Dawa za Tiba Asili Katika Huduma Jumuishi Read More »

NIMR Kuendelea Kuimarisha Tafiti zinazotokana na Mahitaji Halisi ya Wananchi

Tafiti za ndani ya nchi zimekuwa chanzo kikuu cha ushahidi wa kisayansi unaotumika katika kufanya maamuzi ya kisera, kuboresha huduma na kuimarisha mifumo ya afya kwa ujumla. Hayo yamesemwa leo tarehe 4 Aprili na Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti NIMR Dkt. Nyanda Ntinginya, aliyekuwa  akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Taifa ya Utafiti wa Maginjwa ya Binadamu (NIMR) katika mdahalo wa kitaaluma uliohusisha wadau mbalimbali wa afya, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Afya. Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya JKCC- Dodoma kuanzia tarehe 3 hadi 8 Aprili 2025, Dkt. Nyanda amesisitiza nafasi muhimu ya tafiti za kisayansi katika kuboresha huduma za afya nchini Tanzania.“Kujikita katika mbinu za kitafiti kumeleta maendeleo makubwa katika kufikia malengo ya mfumo wa afya – kuanzia kwenye utoaji wa huduma, utawala bora, hadi ushirikishwaji wa wadau katika kuongeza usawa wa huduma za afya nchini Tanzania, NIMR inaendelea kuimarisha tafiti zinazotokana na mahitaji halisi ya wananchi ili kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika kufikia huduma bora za afya,” amesema Dkt. Nyanda.Aidha Dkt. Nyanda amebainisha kuwa mafanikio ya kisera yanayotokana na tafiti za ndani ni pamoja na kuboreshwa kwa uwezo wa watumishi wa afya, mifumo ya usimamizi na taarifa, upatikanaji wa dawa, pamoja na mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.Mbali na kushiriki mdahalo huo wa kitaaluma, NIMR pia inashiriki kwenye maonesho yaliyoandaliwa na Wizara, bandani tuna bidhaa mbalimbali za tiba asili zinazozalishwa na kituo cha Mabibo, tunatoa elimu kuhusu mchakato wa kupata vibali vya utafiti wa afya, na kuonesha kwa vitendo namna tafiti za wadudu waenezao magonjwa kama mbu zinavyofanyika.Ushiriki wa NIMR katika maadhimisho ya Wiki ya Afya ni sehemu ya juhudi za Taasisi katika kuhakikisha Tanzania inafikia lengo la “Afya Kwa Wote”, kwa kutumia tafiti za kisayansi kama nyenzo muhimu.

NIMR Kuendelea Kuimarisha Tafiti zinazotokana na Mahitaji Halisi ya Wananchi Read More »