NIMR

March 9, 2026

Wanawake wa NIMR Mbeya Waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Matendo ya Huruma na Elimu ya Uwiano wa Majukumu ya Kazi na Familia.

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, tarehe 08 Machi, wanawake wa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Mbeya walionyesha mshikamano na kujitolea kwa jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii, matendo ya huruma, na utoaji wa elimu, wakilenga kuimarisha ustawi wa wanawake na makundi yenye uhitaji maalumu. Maadhimisho haya mwaka huu yalibeba kaulimbiu isemayo: “Haki ya Mwanamke na Wasichana, Msingi wa Maendeleo Jumuishi Kufikia Dira 2050.”Maadhimisho hayo yalianza kwa ziara ya kipekee katika kituo cha watoto yatima cha Mountain Glory, kilichopo Pambogo, kata ya Iyela. Watumishi wa NIMR Mbeya walitoa msaada wa vyakula, nguo, na mashine ya kufulia nguo, ili kusaidia kuboresha maisha ya kila siku ya watoto waliokuwa katika kituo hicho.Pia, wanawake hao walitembelea Kituo cha Afya Ruanda kilichopo jijini Mbeya, ambapo walikabidhi mashuka kwa ajili ya wodi ya wazazi. Msaada huo unatarajiwa kuboresha huduma na mazingira ya wagonjwa, hususan akina mama wanaojifungua katika kituo hicho.Siku ya kilele ilijaa elimu na mafunzo. Madaktari na watafiti wa NIMR Mbeya walitoa elimu kwa wanawake kutoka taasisi mbalimbali kuhusu umuhimu wa tafiti za afya na nafasi ya wanawake kushiriki kikamilifu katika tafiti hizo. Lengo lilikuwa kuongeza uelewa na kuhamasisha wanawake kuwa sehemu ya maendeleo ya sayansi na afya katika jamii.Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Dkt. Betrece Ngaraguza aliwafundisha wanawake namna ya kuweka uwiano kati ya majukumu ya kazi, familia, na jamii bila kuathiri afya zao. Alisisitiza kuwa kupanga majukumu kwa uangalifu ni muhimu kulinda afya za kimwili na kiakili.Kwa upande wake, Dkt. Lucy Mrema alitoa mada kuhusu uhusiano kati ya biolojia ya mwanamke na maisha ya kisasa, akisisitiza jinsi maarifa haya yanavyosaidia wanawake kupanga kwa ufanisi kazi, maisha binafsi na familia huku wakihakikisha afya zao zinadumishwa.Naye mlezi wa wanawake wa NIMR Mbeya, Bi. Mwanaharabu Gwato, alisema shughuli hizi ni sehemu ya utamaduni uliojengeka miongoni mwa wanawake wa taasisi hiyo. Alibainisha kuwa wanawake wa NIMR Mbeya wamekuwa na desturi ya kuangalia na kusaidia jamii zenye uhitaji maalumu kama njia ya kurejesha mchango kwa jamii.Maadhimisho haya yamethibitisha kuwa wanawake si tu nguvu kazi katika utafiti na maendeleo ya afya, bali pia ni nguzo muhimu katika kuimarisha ustawi wa jamii kupitia elimu, huduma, na mshikamano. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Wanawake wa NIMR Mbeya Waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Matendo ya Huruma na Elimu ya Uwiano wa Majukumu ya Kazi na Familia. Read More »

Wanawake wa NIMR Waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Kuwasaidia Watoto Yatima.

Katika kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, wanawake wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Tanga wameadhimisha siku hiyo kwa kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha FURAHA, kilichopo Raskazone, jijini Tanga, na kutoa msaada wa mahitaji muhimu kama unga, mchele, mafuta, sabuni za kufulia na za kuogea. Baada ya kukabidhi vitu hivyo, watoto hao walionyesha furaha na shukurani zao kupitia nyimbo na michezo mbalimbali.Maadhimisho haya hufanyika kila tarehe 08 Machi. Mwaka huu, yalikuwa na kaulimbiu isemayo: “Haki ya Mwanamke na Wasichana, Msingi wa Maendeleo Jumuishi Kufikia Dira 2050.”Akizungumza kwenye tukio hilo kwa niaba ya wanawake wa NIMR Tanga, Dr. Veneranda Bwana alisema ni desturi ya wanawake wa NIMR kushiriki katika masuala ya jamii, na akasisitiza kwamba kila siku ni fursa ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wengine. “Siku ya Wanawake Duniani ni fursa ya kusherehekea wanawake, lakini pia ni wakati wa kuonyesha mshikamano na wale walioko kwenye hali ngumu,” alisisitiza Dr. Bwana.Msimamizi wa kituo hicho aliwashukuru wanawake wa NIMR Tanga kwa msaada huo na akakaribisha wadau mbalimbali kuendeleza jitihada za kutoa misaada, akibainisha kwamba watoto hao wanahitaji msaada ili kuendeleza maisha yao. Section Title Mkurugenzi Mkuu NIMR Aridhishwa na Maendeleo ya Utafiti na Huduma Kituo Kidogo cha Gonja. ByErick Mboma March 10, 2026 Uncategorized Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said S. Aboud, ameridhishwa na maendeleo ya shughuli za utafiti na utoaji wa huduma za maabara yanayoendelea… Read More Wanawake wa NIMR Mbeya Waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Matendo ya Huruma na Elimu ya Uwiano wa Majukumu ya Kazi na Familia. ByErick Mboma March 9, 2026 Uncategorized Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, tarehe 08 Machi, wanawake wa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Mbeya walionyesha mshikamano na kujitolea kwa jamii… Read More Wanawake wa NIMR Waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Kuwasaidia Watoto Yatima. ByErick Mboma March 9, 2026 Uncategorized Katika kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, wanawake wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Tanga wameadhimisha siku hiyo kwa kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha FURAHA, kilichopo Raskazone… Read More NIMR Yatoa Matokeo ya Utafiti Kuonyesha Mwelekeo Mpya wa Kujenga Ustahimilivu Dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko Yanayosababishwa na Wadudu Dhurifu ByErick Mboma March 1, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tarehe 26 Februari 2026, kupitia mradi wa RAFT (Resilience Against Future Threats through Vector Control), imewasilisha matokeo ya utafiti… Read More NIMR Director General Strengthens Research Direction at Tanga Centre to Address National Health Priorities ByErick Mboma February 26, 2026 Uncategorized The Tanga Medical Research Centre had the honor of hosting Professor Said Aboud, the Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), on 24th February 2026, during an official… Read More NIMR and EAHRC Launch Landmark National Workshop on Evidence-Based Healthcare ByErick Mboma February 21, 2026 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) in collaboration with the East African Health Research Commission (EAHRC), have launched the 1st National Workshops on Ethics and Clinical Research… Read More NIMR Yazindua Utafiti wa Utoaji wa Dawa ya Kichocho kwa Watoto Chini ya Miaka Mitano Kupitia Mradi wa STEPPES ByErick Mboma February 19, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Mradi wa STEPPS (Strengthening Health System Capacity for Access and Delivery of Paediatric Praziquantel for Schistosomiasis in… Read More NIMR na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Zasaini Hati ya Makubaliano Kushirikiana Katika Tafiti Nchini ByErick Mboma February 13, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe (MNMH) leo tarehe 13/02/2026 zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) inayolenga kuimarisha… Read More NIMR Yawanoa Watumishi wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Kuandika Maandiko ya Utafiti Kuboresha Huduma za Afya ByErick Mboma February 13, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Kituo cha Muhimbili, imewajengea uwezo watumishi wa afya 18 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana (Amana RRH) katika uandishi wa… Read More Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Wanawake wa NIMR Waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Kuwasaidia Watoto Yatima. Read More »