NIMR Yatoa Matokeo ya Utafiti Kuonyesha Mwelekeo Mpya wa Kujenga Ustahimilivu Dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko Yanayosababishwa na Wadudu Dhurifu
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tarehe 26 Februari 2026, kupitia mradi wa RAFT (Resilience Against Future Threats through Vector Control), imewasilisha matokeo ya utafiti kuhusu magonjwa ya mlipuko yanayoenezwa na mbu pamoja na usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu, hatua inayolenga kuimarisha ustahimilivu wa taifa katika kukabiliana na vitisho vya magonjwa hayo.Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Tafiti, Dkt. Nyanda Elias Ntinginya, amesema Tanzania inahitaji kuimarisha mifumo yake ya ufuatiliaji na maandalizi ili kukabiliana kwa ufanisi na ongezeko la vitisho vya magonjwa yanayoenezwa na mbu.Amesisitiza kuwa tafiti za kisayansi zinapaswa kuwa msingi wa maamuzi ya kisera, hasa katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya mazingira, ukuaji wa miji na ongezeko la mwingiliano wa watu vinaongeza hatari ya milipuko ya magonjwa kama dengue na magonjwa mengine ya virusi yanayoenezwa na mbu.Kwa upande wake, Mtafiti Kiongozi wa Mradi wa RAFT, Dkt. Alphaxard Manjurano, amesema lengo la mkutano huo lilikuwa kuwasilisha matokeo muhimu kuhusu usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu na vitisho vya magonjwa ya mlipuko yanayoenezwa na mbu, pamoja na kuyajadili kwa kina na wadau wakuu wa udhibiti wa wadudu dhurifu nchini.Akiwasilisha matokeo ya tathmini ya kitaifa ya utayari wa mfumo wa afya kukabiliana na vitisho vya mbu, Dkt. Manjurano alibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa vituo 34 vya ufuatiliaji wa malaria (sentinel sites), bado kuna haja ya kuanzisha programu mahsusi ya kitaifa ya ufuatiliaji wa kawaida wa mbu wanaoeneza magonjwa.“Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2024, ufuatiliaji wa mbu wa kuanzia hatua za mabuu hadi mbu waliokomaa haujawahi kufanyika kwa mfumo wa kitaifa. Hii inaonesha umuhimu wa kuimarisha mfumo wa utambuzi wa mapema wa hatari za milipuko ya magonjwa ya yanayoenezwa na wadudu,” alisisitiza Dkt. Manjurano.Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya kupitia Programu ya Taifa ya Udhibiti wa Malaria, Bw. Winfred Mwafongo, amesema matokeo hayo yatasaidia kuboresha sera na miongozo ya kukabiliana na malaria na magonjwa mengine yanayoenezwa na wadudu.Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Jovin Kitau, ameipongeza NIMR kwa kufanya utafiti huo, akisema utachangia kuimarisha kinga ya jamii dhidi ya magonjwa yanayoenezwa na wadudu na kuongeza usalama wa afya ya umma.Aidha, Mtafiti Mkuu kutoka NIMR, Dkt. William Kisinza, amesema katika majadiliano ya kikao hicho wadau wamependekeza kuimarishwa kwa programu maalumu inayosimamia masuala ya wadudu dhurifu ili kuongeza ufanisi wa udhibiti wa magonjwa yanayoenezwa na wadudu.Kwa upande wake, Bi. Jackeline Martin, Mtafiti kutoka NIMR aliyefanya utafiti kuhusu ufanisi wa viuatilifu vilivyopo kwenye vyandarua, amesema matokeo yanaonesha ongezeko la usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu hivyo, jambo linaloonesha umuhimu wa kuendelea kuboresha mikakati ya udhibiti ili kuhakikisha vyandarua vinaendelea kuwa na ufanisi.Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Protea, jijini Dar es Salaam, uliwakutanisha wadau mbalimbali wa udhibiti wa wadudu dhurifu kutoka Wizara ya Afya, NIMR, Shirika la Afya Duniani (WHO), Taasisi ya Afya ya Ifakara, pamoja na wadau wengine wa sekta ya afya. Section Title NIMR Yatoa Matokeo ya Utafiti Kuonyesha Mwelekeo Mpya wa Kujenga Ustahimilivu Dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko Yanayosababishwa na Wadudu Dhurifu ByErick Mboma March 1, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tarehe 26 Februari 2026, kupitia mradi wa RAFT (Resilience Against Future Threats through Vector Control), imewasilisha matokeo ya utafiti… Read More NIMR Director General Strengthens Research Direction at Tanga Centre to Address National Health Priorities ByErick Mboma February 26, 2026 Uncategorized The Tanga Medical Research Centre had the honor of hosting Professor Said Aboud, the Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), on 24th February 2026, during an official… Read More NIMR and EAHRC Launch Landmark National Workshop on Evidence-Based Healthcare ByErick Mboma February 21, 2026 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) in collaboration with the East African Health Research Commission (EAHRC), have launched the 1st National Workshops on Ethics and Clinical Research… Read More NIMR Yazindua Utafiti wa Utoaji wa Dawa ya Kichocho kwa Watoto Chini ya Miaka Mitano Kupitia Mradi wa STEPPES ByErick Mboma February 19, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Mradi wa STEPPS (Strengthening Health System Capacity for Access and Delivery of Paediatric Praziquantel for Schistosomiasis in… Read More NIMR na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Zasaini Hati ya Makubaliano Kushirikiana Katika Tafiti Nchini ByErick Mboma February 13, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe (MNMH) leo tarehe 13/02/2026 zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) inayolenga kuimarisha… Read More NIMR Yawanoa Watumishi wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Kuandika Maandiko ya Utafiti Kuboresha Huduma za Afya ByErick Mboma February 13, 2026 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kupitia Kituo cha Muhimbili, imewajengea uwezo watumishi wa afya 18 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana (Amana RRH) katika uandishi wa… Read More WRAIR Delegation Visits NIMR–Mbeya Centre to Advance HIV Research Collaboration ByErick Mboma February 12, 2026 Uncategorized The National Institute for Medical Research – Mbeya Medical Research Centre (NIMR-MMRC) on 10th February 2026 hosted a high-level delegation from Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) in a… Read More Matokeo ya utafiti wa EPInA yaonesha kupungua kwa usubi na kifafa Mahenge ByErick Mboma February 7, 2026 Uncategorized Kiwango cha ugonjwa wa usubi kwa watu wenye kifafa katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, kimepungua hadi asilimia 22, huku maambukizi kwa ujumla yakipungua kwa takribani asilimia… Read More NIMR Emerges as a Global and Regional Leader in EDCTP-Supported Health Research ByErick Mboma January 12, 2026 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) in Tanzania, has been recognized as a leading contributor to internationally competitive health research following its strong performance in… Read More Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.
