Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

August 15, 2026

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Henry M. Jackson Foundation (HJF) ya Marekani zimejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za pamoja, kuimarisha uwezo wa watafiti na kutumia miundombinu iliyopo kupanua wigo wa tafiti nchini.Majadiliano hayo yalifanyika tarehe 13 Agosti 2026 katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya, wakati Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa HJF, Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Marekani, Dkt. Joseph Caravalho, pamoja na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, alisema kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani kunatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano katika tafiti za afya, hasa wakati ambapo mazingira ya ufadhili wa tafiti za afya duniani yanaendelea kubadilika.Prof. Aboud alisema NIMR imewekeza katika miundombinu ya utafiti katika Kituo cha Mbeya na vituo vyake vingine, ikiwemo maabara na vifaa vinavyowezesha tafiti mbalimbali za afya.Katika majadiliano hayo, pande hizo pia zilizungumzia mabadiliko katika ufadhili wa utafiti kutoka Marekani. Prof. Aboud alitoa shukrani kwa Serikali ya Marekani kwa mchango wake kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), ambao umeunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na changamoto nyingine za afya ya umma.NIMR na HJF pia zilijadili maeneo ya ushirikiano wa baadaye, yakiwemo kuendeleza tafiti za pamoja, kujenga uwezo wa watafiti na kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano wa kisayansi.Baada ya majadiliano, ujumbe wa HJF ulitembelea Maabara ya Usalama na Kinga ya Mwili (Safety and Immunology) ya Kituo cha NIMR Mbeya, ambapo ulijionea shughuli za utafiti zinazotekelezwa katika kituo hicho. Ujumbe huo pia ulielezwa kuhusu uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo HJF, katika kuimarisha miundombinu ya kituo.Ziara hiyo ilihitimishwa kwa pande zote mbili kueleza utayari wa kuendeleza ushirikiano uliopo na kutumia miundombinu na uwezo wa watafiti kupanua tafiti za afya nchini. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR na HJF Kuimarisha Ushirikiano wa Tafiti za Afya Read More »

NIMR and HJF Strengthen Health Research Collaboration

The National Institute for Medical Research (NIMR) and the U.S.-based Henry M. Jackson Foundation (HJF) have discussed strategies to strengthen the existing collaboration in health research including joint research, capacity building for researchers, and making better use of existing infrastructure to expand the scope of health research in Tanzania.The discussions took place on 13th August 2026 at the NIMR Mbeya Research Centre, during a visit by HJF President and Chief Executive Officer, retired U.S. Army Major General Dr. Joseph Caravalho, and his delegation.Speaking during the visit, NIMR Director General Prof. Said Aboud said the signing of the Memorandum of Understanding (MoU) between the Governments of Tanzania and the United States provides an opportunity to further strengthen bilateral cooperation in health research, particularly at a time when the global health research funding landscape is changing.Prof. Aboud noted that NIMR has invested in research infrastructure at the Mbeya Research Centre and its other centres, including laboratories and equipment that support a range of health research activities.The discussions also covered changes in U.S. research funding. Prof. Aboud expressed appreciation to the U.S. Government for its support through the President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), which has contributed to Tanzania’s efforts to address HIV and other public health challenges.NIMR and HJF also discussed areas for future collaboration, including joint research, researcher capacity building and identifying new areas of scientific cooperation.Following the discussions, the HJF delegation visited the Safety and Immunology Laboratory at the NIMR Mbeya Research Centre, where they observed ongoing research activities. The delegation was also briefed on investments made by the Government in collaboration with various partners, including HJF, to strengthen the Centre’s research infrastructure.The visit concluded with both sides expressing their commitment to continuing the existing partnership and making use of available infrastructure and research capacity to expand health research in Tanzania. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR and HJF Strengthen Health Research Collaboration Read More »

Dira 2050