NIMR Yasisitiza Tafiti Zinazotatua Changamoto za Afya Katika Maandalizi ya Bajeti ya 2026/2027

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said Aboud, ameitaka taasisi hiyo kuimarisha uwezo wake wa kifedha na kuwekeza katika tafiti zinazolenga kutatua changamoto za afya nchini, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.Akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha maandalizi ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 11 Machi 2026 katika Hoteli ya Edema mjini Morogoro, Profesa Aboud alipongeza ushiriki mkubwa wa wataalamu wa bajeti kutoka kurugenzi, vitengo na vituo mbalimbali vya taasisi.“Kikao kazi hiki kimeonesha kwa vitendo dhana ya ushirikishwaji wa wadau muhimu katika mchakato wa maandalizi ya bajeti, huku kikizingatia miongozo ya serikali katika upangaji wa mipango na matumizi ya rasilimali za taasisi,” alisema.Aliwataka washiriki kuhakikisha kuwa katika kupanga bajeti wanatanguliza vipaumbele vya taasisi kwa kutenga rasilimali za kutosha katika maeneo muhimu yatakayochangia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuiwezesha taasisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. Alieleza kuwa ni wakati muafaka kwa taasisi kuangalia namna ya kufanya tafiti zinazolenga kutatua changamoto za afya nchini kupitia vyanzo vyake vya mapato ya ndani na kupunguza utegemezi.Alielekeza timu inayohusika na mipango na bajeti kuangalia uwezekano wa kutenga fedha za awali za tafiti (research seed fund) ili kuwasaidia hasa watafiti wachanga kuanzisha tafiti zitakazochangia maendeleo ya sekta ya afya nchini. Ametoa wito pia kwa taasisi kuanzisha mfuko wa fedha wa kuwezesha kufanya tafiti za afya (Research endowment fund).Vilevile, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha ustawi wa watumishi, akiiagiza timu hiyo kuangalia uwezekano wa kutekeleza kipengele cha posho ya chakula kwa watumishi kwa mujibu wa mpango wa motisha ambapo kwa sasa hulipwa nauli pekee wakati wa shughuli rasmi za kikazi.Kikao kazi hicho kiliwakutanisha maafisa bajeti kutoka vituo, kurugenzi na vitengo mbalimbali vya NIMR kwa lengo la kuandaa mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali na taasisi. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

NIMR Yasisitiza Tafiti Zinazotatua Changamoto za Afya Katika Maandalizi ya Bajeti ya 2026/2027 Read More »