Wizara ya Afya Yazindua Baraza la Nimr Jipya
Wizara ya Afya leo tarehe 26/09/2025 imezindua Baraza jipya la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), hatua muhimu inayolenga kuimarisha utafiti wa kisayansi, kukuza ubunifu na kuhakikisha mafanikio ya Taasisi kwa ustawi wa watanzania. Akizindua Baraza hilo katika ofisi ndogo za NIMR Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, amesisitiza umuhimu wa Baraza kutoa ushauri wa kitaalamu, kusimamia utendaji wa NIMR, na kuhakikisha matokeo ya tafiti yanachangia kuboresha huduma za afya nchini.Aidha Dkt. Shekalaghe amesisitiza kuwa ushirikiano baina ya Baraza, Menejimenti na Wizara ya Afya ni muhimu ili kuimarisha tafiti za afya na kuhakikisha matokeo yanatumiwa ipasavyo katika kutatua changamoto za kiafya za wananchi.Akimkaribisha Katibu Mkuu kuzindua Baraza, Mwenyekiti wa Baraza jipya Prof. James Mdoe, ameahidi kuliongoza Baraza kwa weledi na uadilifu, akisisitiza kuwa litahakikisha NIMR inatoa ushauri sahihi kwa Serikali. Amesema pia Taasisi itatumia teknolojia za kisasa na fursa za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolution) kuongeza tija katika shughuli za utafiti.โMheshimiwa Katibu MkuuTunapenda kukuhakikishia kuwa, tupo tayari kwa kazi. Tutaweka juhudi zaidi na maarifa katika kutoa mchango wetu wa ushauri kwa mapana zaidi ili Taasisi iendelee kufanya kazi zake kwa ubora zaidi siku hadi siku ili kufikia malengo yake kwa faida ya Watanzaniaโ. Amesisitiza Prof. Mdoe Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, aliwasilisha mafanikio ya Taasisi kwa kipindi cha miaka mitatu (2022/23 hadi 2024/25), akibainisha kuwa NIMR imeongeza idadi ya Miradi ya Utafiti na kufikia 150, huku machapisho ya kisayansi yameongezeka hadi 220 kwa mwaka. Aidha, vijarida sera vimefika 40 kwa mwaka lengo likiwa ni kutumika na watunga sera na wafanya maamuzi ili kuboresha huduma za afya nchini.Prof. Aboud pia alibainisha mafanikio katika ubunifu wa tiba ikiwemo ugunduzi na uendelezaji wa broadly neutralizing antibodies (bNab) katika kituo cha NIMR Mbeya kwa ajili ya tiba ya VVU na UKIMWI. Taasisi pia imeboresha utoaji wa vibali vya utafiti na kupunguza muda kutoka miezi mitatu hadi ndani ya mwezi mmoja, kukarabati majengo chakavu ya vituo vya Gonja (Same), Amani Hill (Muheza), Ngongongare (Arusha) na Tabora, kukamilisha kusimika mitambo ya uzalishaji katika kituo cha tiba asili NIMR Mabibo, kupata ithibati ya kimataifa ya majaribio nasibu katika dawa za wadudu dhurifu (Efficacy Studies on Insecticidal Products) toka SANAS katika maabara ya NIMR Amani (Muheza), kuongezeka kwa makusanyo kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na bajeti ya Taasisi kukua kutoka Sh. bilioni 51.5 hadi Sh. bilioni 89.7 bilioni huku ikiongeza rasilimali za ndani kwa ajili ya uendeshaji wa vituo vyake.Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti mpya wa Baraza, wajumbe wapya, Menejimenti ya NIMR pamoja na mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina. Hatua hizi inachagiza umuhimu wa kuendelea kufanya mageuzi ya Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1979. Section Title Wizara ya Afya Yazindua Baraza la Nimr Jipya ByErick Mboma September 28, 2025 Uncategorized Section Title Wizara ya Afya Yazindua Baraza la Nimr Jipya ByErick Mboma September 28, 2025 Uncategorized Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized… Read More CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section Title CARDIOVASCULAR DISEASE SYMPOSIUM ByErick Mboma September 24, 2025 Uncategorized Section… Read More NIMR Yapongezwa kwa Mchango Mkubwa Katika Kukuza Tiba Asili ByErick Mboma August 31, 2025 Uncategorized Wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za tiba asili kupitia tafiti, na uanzishwaji wa kiwanda cha kuzalisha dawa za tiba asili cha NIMR Mabibo kufuatia juhudi kubwa za Serikali kuhakikisha dawa… Read More Tiba Asili Yazidi Kungโara: Tafiti Zaidi Zahitajika ByErick Mboma August 29, 2025 Uncategorized Imeelezwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza tafiti za tiba asili na kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuzalisha dawa za tiba hizo nchini, ili kuongeza tija katika kuboresha huduma za afya kwa… Read More Tanzania to Learn on Traditional Medicine Sector from South Korea ByErick Mboma August 25, 2025 Uncategorized The Ministry of Health and the National Institute for Medical Research (NIMR) together with partner institutions embarked on a study visit to the National Institute for Korean Medicine Development… Read More Ministry of Health, NIMR Visits South Korea to Strengthen Innovation and Product Development in Traditional Medicine ByErick Mboma August 20, 2025 Uncategorized ๐ ๐ถ๐ป๐ถ๐๐๐ฟ๐ ๐ผ๐ณ ๐๐ฒ๐ฎ๐น๐๐ต, ๐ก๐๐ ๐ฅ ๐ฉ๐ถ๐๐ถ๐ ๐ฆ๐ผ๐๐๐ต ๐๐ผ๐ฟ๐ฒ๐ฎ ๐๐ผ ๐ฆ๐๐ฟ๐ฒ๐ป๐ด๐๐ต๐ฒ๐ป ๐๐ป๐ป๐ผ๐๐ฎ๐๐ถ๐ผ๐ป ๐ฎ๐ป๐ฑ ๐ฃ๐ฟ๐ผ๐ฑ๐๐ฐ๐ ๐๐ฒ๐๐ฒ๐น๐ผ๐ฝ๐บ๐ฒ๐ป๐ ๐ถ๐ป ๐ง๐ฟ๐ฎ๐ฑ๐ถ๐๐ถ๐ผ๐ป๐ฎ๐น ๐ ๐ฒ๐ฑ๐ถ๐ฐ๐ถ๐ป๐ฒ The Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), Prof… Read More NIMR, Wizara ya Afya Watoa Mafunzo kwa Wataalamu wa Afya Kutumia Teknolojia ya Uchambuzi na Ufuatiliaji wa Vinasaba vya Magonjwa ya Mlipuko ByErick Mboma August 20, 2025 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa Kushirikiana na Wizara ya Afya, tarehe 18/08/2025 imeanza mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa maabara na watafiti kutoka taasisi… Read More Heri ya Siku ya Wakulima “Nanenane” ByErick Mboma August 8, 2025 Uncategorized Section Title Heri ya Siku ya Wakulima “Nanenane” ByErick Mboma August 8, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR), in partnership with the University of Oslo… Read More NIMR Hosts Pandemic Ethics Project General Assembly, Welcomes Experts from Six Countries ByErick Mboma July 30, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR), in partnership with the University of Oslo, hosted a high-level Pandemic Ethics General Assembly today 30th July 2025, at its Sub Office in Dar es… Read More Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.
Wizara ya Afya Yazindua Baraza la Nimr Jipya Read More ยป
