Tiba Asili Yazidi Kung’ara: Tafiti Zaidi Zahitajika
Imeelezwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza tafiti za tiba asili na kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuzalisha dawa za tiba hizo nchini, ili kuongeza tija katika kuboresha huduma za afya kwa jamii. Kwa sasa, wananchi wengi wameonyesha mwamko mkubwa wa kutumia dawa za tiba asili.Kauli hiyo imetolewa leo, Agosti 29, 2025 na Dkt. Ahmad Mohamed Makuwani Mkurugenzi wa Huduma ya Afya ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Watoto kutoka Wizara ya Afya, alipomuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika Kongamano la Nne la Kisayansi la Tiba Asili lililoandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar, jijini Dodoma.Dkt. Makuani amewataka watafiti na wadau wa tiba asili kuwekeza nguvu katika kupata ushahidi wa kisayansi wa dawa hizo utakaosaidia kuimarisha sera za afya na kukuza ushirikiano kati ya wanasayansi na wataalamu wa tiba asili.“Ili kuendeleza usawa wa afya, ni lazima dawa za tiba asili ambazo zimethibitishwa kuwa salama, zenye ufanisi na ubora ziingizwe rasmi kwenye mifumo ya utoaji huduma za afya. Tanzania tayari imeweka msingi imara kupitia Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya NIMR ya mwaka 1980,” amesisitiza Dkt. Makuani.Aidha, amependekeza kuundwa kwa mifumo ya ushirikiano na rufaa kati ya tiba asili na tiba za kisasa, kujumuisha tiba asili katika miongozo ya matibabu, na kujenga uaminifu kati ya wataalamu wa afya na waganga wa tiba asili.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, amesema taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama, ufanisi na ubora wa dawa za tiba asili, ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa zisizo salama.Prof. Aboud amewataka waganga na wataalamu wa tiba asili kupeleka dawa zao NIMR na katika taasisi zingine zenye mamlaka ili zipimwe na kuthibitishwa. “Hii itawezesha dawa hizo kuwa sehemu ya huduma jumuishi katika hospitali 14 za rufaa nchini,” amesisitiza Prof. Aboud.Kongamano hilo la siku moja limewakutanisha wadau wa tiba asili kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo walijadili matokeo ya tafiti mbalimbali. Kongamano hilo pia limeambatana na Maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika, yaliyofunguliwa Section Title Tiba Asili Yazidi Kung’ara: Tafiti Zaidi Zahitajika ByErick Mboma August 29, 2025 Uncategorized The Ministry of Health and the National Institute for Medical Research (NIMR) together with partner institutions embarked on a study visit to the National Institute for Korean Medicine Development… Read More Tanzania to Learn on Traditional Medicine Sector from South Korea ByErick Mboma August 25, 2025 Uncategorized The Ministry of Health and the National Institute for Medical Research (NIMR) together with partner institutions embarked on a study visit to the National Institute for Korean Medicine Development… Read More Ministry of Health, NIMR Visits South Korea to Strengthen Innovation and Product Development in Traditional Medicine ByErick Mboma August 20, 2025 Uncategorized 𝗠𝗶𝗻𝗶𝘀𝘁𝗿𝘆 𝗼𝗳 𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵, 𝗡𝗜𝗠𝗥 𝗩𝗶𝘀𝗶𝘁 𝗦𝗼𝘂𝘁𝗵 𝗞𝗼𝗿𝗲𝗮 𝘁𝗼 𝗦𝘁𝗿𝗲𝗻𝗴𝘁𝗵𝗲𝗻 𝗜𝗻𝗻𝗼𝘃𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻 𝗮𝗻𝗱 𝗣𝗿𝗼𝗱𝘂𝗰𝘁 𝗗𝗲𝘃𝗲𝗹𝗼𝗽𝗺𝗲𝗻𝘁 𝗶𝗻 𝗧𝗿𝗮𝗱𝗶𝘁𝗶𝗼𝗻𝗮𝗹 𝗠𝗲𝗱𝗶𝗰𝗶𝗻𝗲 The Director General of the National Institute for Medical Research (NIMR), Prof… Read More NIMR, Wizara ya Afya Watoa Mafunzo kwa Wataalamu wa Afya Kutumia Teknolojia ya Uchambuzi na Ufuatiliaji wa Vinasaba vya Magonjwa ya Mlipuko ByErick Mboma August 20, 2025 Uncategorized Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa Kushirikiana na Wizara ya Afya, tarehe 18/08/2025 imeanza mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa maabara na watafiti kutoka taasisi… Read More Heri ya Siku ya Wakulima “Nanenane” ByErick Mboma August 8, 2025 Uncategorized Section Title Heri ya Siku ya Wakulima “Nanenane” ByErick Mboma August 8, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR), in partnership with the University of Oslo… Read More NIMR Hosts Pandemic Ethics Project General Assembly, Welcomes Experts from Six Countries ByErick Mboma July 30, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR), in partnership with the University of Oslo, hosted a high-level Pandemic Ethics General Assembly today 30th July 2025, at its Sub Office in Dar es… Read More NIMR Management Trained on Corporate Entrepreneurship ByErick Mboma July 30, 2025 Uncategorized In a strategic move to enhance institutional sustainability and increase revenue collections, the National Institute for Medical Research (NIMR) has conducted a high-level training on corporate… Read More NIMR Highlights Digital Health Solutions for HIV-Exposed Infants at National Child Health Congress ByErick Mboma July 27, 2025 Uncategorized The National Institute for Medical Research (NIMR) played a pivotal role in the 2nd Tanzania Child Health and Welfare Congress, held from 23rd – 25th July 2025 in Arusha, by spotlighting cutting-edge… Read More Mwenyekiti Mpya wa Baraza la NIMR Aonyesha Dhamira ya Kuimarisha Utafiti wa Afya ByErick Mboma July 26, 2025 Uncategorized Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. James Mdoe, leo tarehe 25 Julai 2025 amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti cha NIMR Muhimbili… Read More
Tiba Asili Yazidi Kung’ara: Tafiti Zaidi Zahitajika Read More »