Wanawake wa NIMR Mbeya Watoa Zawadi kwa Kliniki za Utafiti wa Afya Kusaidia Washiriki
Wanawake wa Kituo cha Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Mbeya wametoa zawadi za mashuka kwa kliniki za utafiti zinazotumiwa na kituo hicho ili kusaidia washiriki wa tafiti mbalimbali za afya, kama ishara ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya utafiti wa afya nchini.Kliniki zilizopokea mashuka hayo ni za utafiti wa kifua kikuu, VVU/UKIMWI pamoja na kisukari inayodhaminiwa na mradi wa PROTID. Mashuka hayo yalikabidhiwa tarehe 18 Aprili, 2026 kwa uongozi wa NIMR Mbeya kwa ajili ya kuwafikishia washiriki wanaohudumiwa kupitia kliniki hizo.Hatua hiyo inalenga kuonyesha kutambua na kuthamini ushiriki wa wananchi ambao wamekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha tafiti za kisayansi zinazolenga kuboresha afya ya jamii.Akizungumza wakati wa kupokea zawadi hizo, Meneja wa Kituo cha NIMR Mbeya, Dkt. Bariki Mtafya, amesema mafanikio ya tafiti nyingi za afya hutegemea ushiriki wa wananchi, hivyo ni muhimu kuendelea kuthamini mchango wao.“Washiriki wa tafiti ni sehemu muhimu ya maendeleo ya sayansi ya afya. Hatua hii inaonesha kuthamini mchango wao na kuimarisha uhusiano kati ya watafiti na jamii,” amesema Dkt. Mtafya.Dkt. Mtafya pia amewapongeza wanawake wa NIMR Mbeya kwa moyo wa kujitolea, mshikamano na ushirikiano wao, akisema wameendelea kuwa chachu ya maendeleo ndani ya taasisi kupitia shughuli mbalimbali zinazounga mkono utafiti.Ameongeza kuwa wanawake wana nafasi muhimu katika kuendeleza sayansi na teknolojia, si tu kama watafiti bali pia kama viongozi na wabunifu wanaochangia mabadiliko chanya katika jamii.Aidha, amesema uongozi wa kituo utaendelea kuunga mkono juhudi za wanawake hao ili waendelee kutekeleza malengo yao ya kuimarisha shughuli za utafiti na ustawi wa jamii.Tukio hilo linaendelea kudhihirisha umuhimu wa ushirikiano kati ya watafiti na jamii katika kuhakikisha tafiti za afya zinafanikiwa na matokeo yake yanawanufaisha Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.
Wanawake wa NIMR Mbeya Watoa Zawadi kwa Kliniki za Utafiti wa Afya Kusaidia Washiriki Read More »
