NIMR

KONGAMANO LA NNE LA KISAYANSI LA TIBA ASILI

29 Agosti, 2025

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ikishirikiana na Wizara ya Afya inapenda kuwaalika waganga wa tiba asili na tiba mbadala, watafiti, wataalamu wa afya katika nyanja mbalimbali, watunga sera, wafanya maamuzi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika Kongamano la Nne la Kisayansi la Tiba Asili litakalofanyika tarehe 29 Agosti 2025, katika Ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma, Tanzania.

Mada kuu ya Kongamano la mwaka huu ni: “Kuboresha Tiba Asili kwa Usawa wa Afya, Ubunifu na Maendeleo Endelevu.”

Ada ya Washiriki wa Kongamano Kiasi
Wataalamu wa Tiba asili na mbadala(Waganga, wauzaji, watengenezaji na waratibu)
TZS 50,000
Washiriki kutoka Afrika Mashariki
TZS 150,000
Washiriki nje ya Afrika Mashariki
TZS 400,000
Wanafunzi wa Afrika Mashariki
TZS 50,000
Wanafunzi nje Afrika Mashariki
TZS 130,000

Malipo yote yafanyike kwenye control namba 995910068968 yenye jina la mlipaji NATIONAL INSTITUTE FOR MEDICAL RESEARCH

Kongamano hili litaambatana na maonesho ya wiki ya tiba asili ya Mwafrika, yatakayofanyika kuanzia Tarehe 25-31 Agosti 2025 kwenye Viwanja vya Chinangali. Mwisho wa usajili ni tarehe 15 Agosti 2025

Washiriki watakaowasilisha mada katika Kongamano wanaombwa kuwasilisha Ikisiri (Abstract) na mwisho wa kuwasilisha ni tarehe 15 Agosti 2025

Kwa maelezo zaidi piga simu +255 782 595 150