Jumla ya watumishi wapya 41 wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kutoka kada 11 tofauti wamehitimisha mafunzo elekezi ya siku nne yaliyolenga kuwaandaa rasmi kwa majukumu yao ndani ya utumishi wa umma.
Mafunzo hayo yalifanyika kuanzia tarehe 8 hadi 11 Aprili, 2025 katika Ukumbi wa CEEMI uliopo Ofisi ndogo za NIMR jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof. Said Aboud alieleza matumaini makubwa juu ya mchango wa watumishi hao wapya katika kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi. “Tunaamini kuwa kupitia mafunzo haya, tumepata watumishi wenye weledi, maadili na ari ya kufanya kazi kwa bidii, kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za Serikali,” alisema Prof. Aboud.
Miongoni mwa mada muhimu zilizofundishwa ni pamoja na taratibu za utumishi wa umma, sheria za kazi, utunzaji wa siri za Serikali, haki na wajibu wa mtumishi, muundo wa Taasisi na namna bora ya kutekeleza majukumu kwa uadilifu na weledi.
Mafunzo yalitolewa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Usalama wa Serikali (GSO) sambamba na wakurugenzi wa idara mbalimbali za NIMR akiwemo Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti (DRCP), Mkurugenzi wa Taarifa na Kurekebu Tafiti (DRIRA), Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi pamoja na wakuu wa Idara ya Uhasibu, Ukaguzi wa Ndani, na TEHAMA.
Katika kilele cha mafunzo hayo, watumishi wamekula kiapo cha uadilifu ambayo ni ishara ya dhamira ya dhati ya kuwahudumia watanzania kwa uaminifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
NIMR inaendelea kuwekeza katika kuimarisha rasilimali watu kwa kuwajengea uwezo watumishi wake mara wanapojiunga ili kuhakikisha wanaanza kazi wakiwa na uelewa mpana wa majukumu yao na mchango wao katika kufanikisha malengo ya Taasisi