Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imepiga hatua katika kuboresha miundombinu ya Kituo cha Utafiti cha Tukuyu baada ya kukamilika kwa sehemu kubwa ya kazi za ukarabati wa awamu ya kwanza, hatua inayolenga kuimarisha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi wa shughuli za utafiti.
Ukarabati huo unatekelezwa kwa kutumia vyanzo vya ndani vya mapato vya Taasisi. Katika awamu ya kwanza, kazi zilizotekelezwa zimehusisha kubadilisha mabati ya zamani na kuweka mapya ili kuimarisha paa la jengo na kuondoa changamoto ya kuvuja, kubadilisha dari (ceiling boards) zilizokuwa zimeharibika, kuziba nyufa kwenye kuta na kupaka rangi sehemu za ndani na nje ya jengo.
Aidha, maboresho mengine yaliyofanyika ni pamoja na kuboresha chumba cha maabara kwa kuweka meza na sehemu maalumu za kufanyia kazi zilizotengenezwa kwa marumaru (marble) na kukarabati miundombinu ya umeme.
Kwa upande wake, Mkuu wa kituo cha NIMR Tukuyu, Dkt. Godlisten Shedrack Materu ameishukuru kwa Menejimenti ya Taasisi kwa ushirikiano, usimamizi, maelekezo na kuwezesha utekelezaji wa ukarabati huo. Amesema maboresho hayo ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza uwezo wa kituo kutekeleza majukumu yake ya utafiti.
Kituo cha Utafiti cha NIMR Tukuyu kinashiriki katika tafiti mbalimbali za afya, ikiwemo tafiti zinazohusu ugonjwa wa Usubi. Uboreshaji wa miundombinu yake unatarajiwa kuimarisha mazingira ya utekelezaji wa tafiti hizo na kuongeza mchango wa NIMR katika kuzalisha ushahidi wa kisayansi kwa ajili ya kuboresha afya ya jamii nchini.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.






