Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imefanya ziara ya kijamii tarehe 6 Mei 2025 katika Gereza Kuu la Isanga na Shule ya Viziwi Dodoma, ambapo imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwafariji na kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii.
Msaada huo ulijumuisha magodoro, shuka, dawa za meno, sabuni za kuogea, mafuta ya kupaka, vyakula kama mchele, unga wa ugali, maharage, mahindi, nyama, sukari, mafuta ya kupikia, mikate, unga wa lishe na maziwa ya kopo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala, Bi. Bupe Ndelwa, alieleza kuwa Taasisi inaguswa na hali ya makundi hayo maalumu na kuona umuhimu wa kuwafariji na kuwaonesha 0upendo. Alisisitiza kuwa NIMR kama sehemu ya jamii iliona ni vyema kutumia kidogo walichokuwa nacho kuwafikia ndugu zao ili wasijihisi wametengwa na jamii na kuwatia moyo kuwa wapo pamoja nao na wanawapenda.
Mkuu wa Gereza la Isanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Zephania Neligwa, aliishukuru NIMR kwa moyo wa huruma waliouonesha na kusisitiza umuhimu wa Taasisi na watu binafsi kuwa na utamaduni wa kusaidia makundi yenye uhitaji. Alisema, “Nawapongeza NIMR kwa hatua hii ya kugusa maisha ya wahitaji. Msaada huu si tu unaleta faraja kwa wafungwa, bali pia unaakisi uzalendo na upendo kwa jamii. Msipate hofu ya kutembelea magereza, ni sehemu rafiki, tunawakaribisha kuwatembelea ndugu zetu”.
Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza la Isanga, Sehemu ya Wanawake, Mrakibu wa Magereza Sifa Anyimike, alisema misaada kama hiyo husaidia kupunguza gharama kwa Serikali katika uendeshaji wa magereza na kuhakikisha mahitaji ya msingi ya wafungwa yanatimizwa.
Baada ya ziara hiyo gerezani, NIMR pia ilitembelea Shule ya Viziwi Dodoma na kutoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Awadhi Mbogo, aliipongeza NIMR kwa kujitoa kwao na kuwataka kuendeleza moyo huo wa kutoa pale inapohitajika. “Hili ni tendo la kiutu ambalo limewagusa sana watoto wetu, huku hatufikiwi mara kwa mara, lakini NIMR mmefanya jitihada za kutufikia. Tunawashukuru kwa upendo wenu na tunawaombea muendelee kuwa na moyo wa huruma kwa jamii.” Alisema Mbogo.
Misaada hiyo ni sehemu ya juhudi za taasisi kurudisha kwa jamii na kuonyesha mshikamano na upendo kwa makundi maalumu.