Skip to content
Coat of arms of Tanzania

National Institute for Medical Research (NIMR)

Advancing Health Research, Enhancing Life

NIMR

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendesha warsha ya kupitia vijarida sera (Policy Briefs) na kuviweka tayari kwa kuviwasilisha Wizara ya Afya, iliyoanza tarehe 17 Novemba 2026, Mkoani Morogoro.

Warsha hiyo ni mwendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watafiti wa afya nchini yaliyotolewa hivi karibuni na NIMR. Mafunzo hayo yalilenga kuwaimarisha katika uandishi wa vijarida sera unaozingatia ushahidi wa kisayansi.

Vijarida sera hivyo vinatarajiwa kutoa ushahidi wa kisayansi, taarifa na mapendekezo yatakayosaidia Wizara ya Afya kufanya maamuzi sahihi na kuweka vipaumbele katika kushughulikia masuala muhimu ya afya ya jamii.

Kupitia hatua hiyo, NIMR inalenga kuimarisha matumizi ya matokeo ya tafiti katika uundaji na uboreshaji wa sera za afya, kwa lengo la kuchangia maboresho ya huduma za afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Dira 2050