Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeandaa Mpango wa Manunuzi kwa mwaka wa fedha 2026/27, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika manunuzi ya umma na kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za utafiti unafanyika kwa tija.
Kikao kazi cha maandalizi ya mpango huo kilianza tarehe 18 Mei 2026 kikihusisha wataalamu wa manunuzi, wateknolojia wa maabara, wahasibu, watafiti na wataalamu wa mipango, ufuatiliaji na tathmini wakiwakilisha vituo, vitengo na kurugenzi tatu za taasisii kwa lengo la kuandaa mpango wenye uhalisia unaoendana na bajeti na mahitaji katika utekelezaji wa kazi za utafiti.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, amesisitiza umuhimu wa kuandaa mpango wa manunuzi kwa umakini mkubwa na kuzingatia uwezo halisi wa kifedha ili kuepusha changamoto za mpango kutotekelezeka kwa kiwango kilichokusudiwa.
Ameelekeza maafisa manunuzi na ugavi kujiridhisha na mpango na bajeti za kila kitengo kabla ya kuingiza taarifa kwenye mfumo wa NeST, hatua ambayo amesema itasaidia kuongeza uwiano kati ya mpango na rasilimali fedha zilizopo.
Mpango huo unatarajiwa kuwezesha upatikanaji wa bidhaa na huduma muhimu kwa wakati, huku ukizingatia sheria, taratibu, kanuni na mahitaji halisi ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo katika mwaka wa fedha 2026/27.
Wizara ya Afya Tanzania imeendelea kusimamia na kuhimiza matumizi bora ya rasilimali za umma katika taasisi zake kwa lengo la kuboresha huduma za afya nchini.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

