Mamia ya wananchi wamemiminika katika Banda la NIMR kujipatia Kinywaji lishe cha NIMREVIT kwenye wiki ya Afya Kitaifa, iliyofanyika tarehe 3-8 Aprili 2025, kwenye viwanja vya JKCC-Dodoma, ambacho hutengenezwa Kwa mimea ya asili na Kituo cha NiMR Mabibo, ambapo umati huo unathibitisha Imani ya wananchi Kwa Taasisi.
Kinywaji hiki hutengenezwa Mahususi kwaajili ya kuimarisha afya ya mwili kikiwa na faida nyingi kama kuongeza damu, kuimarisha afya ya moyo na mishipa ya damu, kuimarisha mifupa na mishipa ya fahamu, na kuondoa uchovu wa mwili.